Na Luqmani maloto
Mfano wa uhusiano wa Sherry na Mosses ambao tulianza nao wiki iliyopita katika mada hii, tunaukamilisha leo katika sehemu ya mwisho ya makala haya.
Kama tulivyoona, ipo wazi kuwa Mosses ndiye huonesha hisia zake kwa Sherry na hata marafiki zao hufikia kusema kwamba jamaa ndiye anayesababisha uhusiano wao uendelee kuwepo, vinginevyo wangekuwa wamekwishapigana mwereka.
Sherry anapoambiwa amependeza anajibu ‘asante’ halafu imetoka. Akiambiwa yeye ni mwanamke mzuri jibu ni ‘thank you’. Hathubutu kumwambia Mosses kuwa amependeza au ni mwanaume anayemvutia kuliko wote, ila akiwa kazini kwake, pongezi huzimwaga huko. “James umependeza!” Sherry anamwambia mfanyakazi mwenzake.
Wakati mwingine Sherry anakosa hekima, anamueleza Mosses: “Unajua sisi pale kazini kwetu kuna vijana wazuri. Unajua Jamal ana sura nzuri sana? Halafu Sam anajua kupigilia mavazi ukimuona hadi raha.”
Inawezekana Sherry anazungumza kweli lakini kichwani kwake kuna kelele za ndani (internal noises) zinazomsababishia umapepe, hivyo kukosa busara ya kuchagua maneno mbele ya mpenzi wake.
Ukitaka kujua mkuki kwa nguruwe, siku moja Sherry alikutana na Zawadi ambaye ni mfanyakazi mwenzake Mosses. Zawadi akaamua kuwa mkweli: “Mosses nimemuacha ofisini ila kanifurahisha, amenisifia huyo. Anasema nimependeza sana leo.” Ilikuwa ni kama Zawadi kamroga Mosses kwani Sherry alikasirika mno siku hiyo.
Walipokutana nyumbani, Sherry alitaka maelezo ni kwa nini alimsifia Zawadi kwamba amependeza badala ya sifa hizo kuzielekeza kwake. Mosses akaona mpenzi wake anampanda kichwani, akamjibu: “Mbona wewe huwa unawasifia wanaume wa kazini kwako mimi sisemi, tena mbele yangu.” Sherry ikamgonga kichwani, akapata pointi!
Sherry hakujua kwamba sifa alizokuwa anazimwaga kwa wanaume wa kazini kwake ilikuwa sawa na kuchezea hisia za Mosses. Haikumgonga kichwani kwamba anamuumiza mwenzake. Alipokutana na Zawadi na ikawa maumivu kwake. Kila mtu anatakiwa kujali, kusifu kwa sababu hivyo ni vionjo muhimu kwenye mapenzi.
Kama hukubali kwa jinsi mwenzi wako alivyo ni bora kuachana naye kuliko kupotezeana muda. Tambua kuwa usipomsifu wewe anapokwenda atasifiwa halafu ukisikia itakuuma. Wewe humuelezi kama ni mzuri, anapokwenda wapo watakaomuona watamwambia anavutia, je, hapo huoni kama utakuwa umepoteza kura kwa mwenzi wako?
Zaidi ya hayo, kuna vipengele vifuatavyo vya kuzingatia;

ITAKUONGEZEA MVUTO
Ukiwa unamjali na unamsifu, atajua unamkubali kwa jinsi alivyo. Hii itakuongezea ‘maksi’ za kuzidi kukupenda.
UTABORESHA PENZI
Pengine huko alikokuwa hakuwahi kumwagiwa sifa. Ukimjali na kumuonesha jinsi unavyomkubali kwa kumtamkia na vitendo, itamfanya akuone wewe ni mteule uliyeletwa na Mungu kwake. Atakupenda zaidi.

ITAMJENGA KUJIAMINI
Ukimwambia yeye ni mzuri na unampenda sana. Ukimsifia kwa mavazi yake na muonekano wake kwa jumla, itamfanya ajiamini. Hatakuwa na shaka yoyote juu yako. Hata akipita barabarani atajiona yupo kamili. Atakuheshimu!

INAPUNGUZA UWEZEKANO WA KUKUSALITI
Kuna watu husalitiwa si kwa sababu ya kuona wazuri pembeni, ila kwa tabia zao. Wewe hata siku moja humuoneshi kama unamjali, wala humwambii kuwa anavutia. Matokeo yake anakutana na mtu pembeni anayejua kumwaga sifa, anaanza kumuona bora kuliko wewe.

Anamjali na anamsifia kwamba ni mzuri, akivaa anamueleza anavutia. Wewe na ububu wako au uchoyo wa pongezi atakuacha. Atadandia gari la mtu anayejua nini maana ya mapenzi na anayefahamu jinsi ya kucheza na hisia.
Hivyo basi, ukimjali na kumwagia pongezi inavyotakiwa, uwezekano wa yeye kukusaliti utapungua.
UTAKITEKA KICHWA CHAKE
Atake nini tena? Kama ni kujali, wewe unamjali sana, sifa anazipata za kutosha kutoka kwako kwahiyo hatokuwa na shaka yoyote juu yako kwa maana utakuwa umemteka kwa kiwango cha kutosha.
Atake nini tena? Kama ni kujali, wewe unamjali sana, sifa anazipata za kutosha kutoka kwako kwahiyo hatokuwa na shaka yoyote juu yako kwa maana utakuwa umemteka kwa kiwango cha kutosha.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment