ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 11, 2012

MZEE KIPARA HATUNAE TENA

Mzee Fundi Said Enzi Ya Uhai Wake
MSANII mkongwe wa maigizo na filamu, Mzee Fundi Said, aliyevuma katika fani hiyo tangu akishiriki uigizaji vipindi vya Radio Tanzania hadi kundi la Kaole, amefariki leo asubuhi majira ya saa 3:30 huko Kigogo. Hali ya msanii huyo ilianza kuwa ya utata miaka ya karibuni akisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kimwili ambapo jana hali yake ilikuwa mbaya wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika makazi yake katika nyumba inayomilikiwa na kundi la Kaole.

1 comment:

lulu ibrahim said...

inalillah wainallihh rajiun mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi AMIN