Mfalme wa mipasho, Mzee wa kulambisha akipagawisha Mont Vernon, New York kwenye Show kabambe Jumamosi Janauary 21, 2012 iliyokonga nyoyo za mashabiki kwa kuimba nyimbo zake kwa ustadi mkubwa huku akiwa mcheshi muda wote.
Juu na chini ni meza ya Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.
Kulia ni Balozi wa Somalia Umoja wa Mataifa Mh. Dr.Elmi Ahmed Dualeh akiwa na mke wake wakipiga picha ya pamoja na Mzee Yusuf, Mh. Dr. Elmi Ahmed Dualeh alishawahi ishi Zanzibar enzi hizo wakati Mzee Yusuf alipokua mdogo.
Mzee wa alamba, Haaam, Haaam akifanya makamuzi New York.
Mashabiki waliokuja kulambishwa wakichenguka na huku wakimtunza Mzee Yusuf aliyekonga nyoyo zao kwa show iliyofana iliyofanyikia Mont Vernon, New York.
Juu na chini mashabiki wa New York na Vitongoji vya jirani wakiendelea kulambishwa na Mzee Yusuf.
Ilikua balaa hakuna kukaa chini Mzee wa Alamba, Mfalme wa mipasho alivyofunika New York.
Mashabiki wakiimba pamoja na Mzee Yusuf
Ilikua si mchezo uliyekosa karibu DC Feb 4 atalambisha mashabiki wa DMV.
Mashabiki wa New York na Vitongoji vyake wakipagawika na Mzee Yusuf, Mfalme wa mipasho.
Mashabiki wakilambishwa na Mzee Yusuf alipofanya show Mjini New York Jumamosi January 21, 2012.
9 comments:
hihihi hivi kweli ni vijimambo si mchezo hao walovaa vimini ndio wameipendeszesha shoo yote je washaolewa?
Hakuna chochote taarabu na nguo fupi wapi na wapi, njoo pwani uone taarabu inavazi gani
Kweli shoga mwenzio nasafisa dhahabu zangu hapa mana taharab shurti kwa madhaabu na maddish dash au walao nguo ndefu vimini vya disco au sio?
Ni kweli kabisa Taaraba ama kwa jina lingine (Rusha Roho) huvaliwa nguo ndefu kabisaa. We uliyesema waliovaa nguo fupi ndo waliopendezesha umechemsha labda una sababu zako tu. Mzee Yusufu tayari ana Wake zake Bongo wenye Nguo Fupi wanajisumbua tu zaidi ya kujidhalilisha. DMV muwaonyeshe Makali wa New York.
who carezzzzzzzzz? is all about having fun. na kweli tulikula happy kwa raha zetu. Mao you need to REWINDDDDDDDDD.
hiyo ilikuwa wana day thing...more like kwenda kumuona mwimbaji,sio wote walokuwa hapo ni wana taarab,hata perfomance ilikuwa sio kama ya kawaida na wapambe wake,kwahiyo ni watu kukutana,kumuona mwimbaji wabongo na kufurahi...watu wamevaaje hilo si tatizo,nyie wivu umewashika sijui wenzenu wamependeza,watoto wazuriiiiiiii...wamtake mzee yusuf watu wana watu wao na shughuli zao,akili za watu wajinga utazijua tu,kuwaza kutakana tu,watu wazima hovyoooooooooooo....watu wamekula raha zao,wenye wivuna wajinyonge....kulamba wamelambishwa..mtajijuuuuuuuuuuuuu
Don't be jelaous to those people having good time anyway it is New York not Pwani so why they can wear mini dresses daaah!!!
watu bwana, oh mzee yusuph ana wake zake tz, hivi hapo unamuona haswa huyo anaetaka kuwa mke wa mzee yusuph labda kama una miaka hamsini, msijidanganye watu walikuwa wanakula raha tu hapo hakuna amtakae mzee yusuph ovyooooooo
ushamba tu, kunii kuvaa nguo fupi ndo kumtaka mtu. mambo yakiswahili hayo. mpo kiwanja acheni majungu pumbavuuuu
Post a Comment