Fidelis Butahe na Geofrey Nyang’oro
LICHA ya kuvuliwa uanachama na vyama vyao, wabunge Hamad Rashid (Wawi) na David Kafulila (Kigoma Kusini) jana walihudhuria vikao vya Kamati za Bunge na kusema kwamba kitendo cha kutajwa kwamba wao ni wabunge wa Mahakama ni kejeli. Kama kawaida, wabunge hao walifika katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam saa 3 asubuhi huku wakionekana wenye furaha na kusalimiana na wabunge mbalimbali.
LICHA ya kuvuliwa uanachama na vyama vyao, wabunge Hamad Rashid (Wawi) na David Kafulila (Kigoma Kusini) jana walihudhuria vikao vya Kamati za Bunge na kusema kwamba kitendo cha kutajwa kwamba wao ni wabunge wa Mahakama ni kejeli. Kama kawaida, wabunge hao walifika katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam saa 3 asubuhi huku wakionekana wenye furaha na kusalimiana na wabunge mbalimbali.
Desemba 17 mwaka huu, Halmashauri Kuu ya NCCR - Mageuzi katika kikao chake cha dharura kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin, Dar es Salaam, ilimfukuza uanachama Kafulila na wenzake sita akiwamo pia mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.
Hata hivyo Kafulila ambaye alivuliwa uanachama wa chama hicho kwa madai ya kukutwa na hatia ya kutoa siri za chama kwenye vyombo vya habari alifungua kesi Mahakama Kuu ambayo ilitoa zuio la utekelezaji wa uamuzi ya Nec ya chama hicho mpaka kesi hiyo ya msingi itakapomalizika. Kwa upande wa Hamad, Januari 4 mwaka huu zaidi ya robo tatu ya wajumbe wa Baraza Kuu la CUF, walipitisha azimio la kumfukuza uanachama pamoja na wenzake watatu.
Hamad alikumbwa na rungu hilo baada ya kutangaza kumng'oa Katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad. Uamuzi wa mkutano huo ulilalamikiwa na Hamad ambaye alisema kuwa uamuzi huo ulifanyika wakati akiwa amewasilisha barua ya zuio la mahakama,ambayo ilikitaka chama hicho kutoendelea na kikao hicho.
Wabunge hao jana walihudhulia Kamati za Bunge kama kawaida huku Kafulila akisema kuwa kitendo cha kuitwa kuwa ni Mbunge wa Mahakama ni kejeli. “Kusema kuwa kuna wabunge wa mahakama ni kauli ya kejeli kwani mahakama haina majimbo wala viti maalumu…, wako wabunge wa viti maalumu, majimbo na kuteuliwa na rais” alisema Kafulila.
Kwa upande wake, Hamad alisema kuwa yeye ni mbunge kama kawaida kwa kuwa CUF ikikaidi kutekeleza zuio la Mahakama na kuamua kuendelea na kikao ambacho kilimvua uanachama. “Hivi ninavyokwambia wananchi wa jimbo langu wamepanga kufanya maandamano na yatafanyika Januari 19, siku ambayo nitakuwa na kesi mahakama dhidi ya CUF hivyo sitakuwapo katika maandamano hayo watakuwapo wapiga kura wangu” alisema Hamad.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali za Mitaa (LAAC), Augustine Mrema alisema kamati hiyo inatambua kuwa Kafulila bado mjumbe halali wa kamati hiyo kwa sababu sababu haijapata maelezo yoyote kutoka Ofisi ya Spika wa Bunge.
“Swali kama hili ilikuwa aulizwe Spika wa Bunge(Makinda) sio mimi ,Spika ndiye anayeteua wajumbe wa kamati na pia ndiye mwenye uwezo wa kutengua nafasi zao,”alisema Mrema alipoulizwa mmsimamowake juu ya mbunge huyo. Alisema kutokana na hali hiyo kamati yake itaendelea kumtambua mbunge huyo aliyefukuzwa na chama chake cha NCCR Mageuzi hadi hapo Spika atakapotoa maelekezo.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment