ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 21, 2012

WANAFUNZI WA KIISLAM WAANDAMANA DAR KUPINGA KUFUKUZWA KWA WENZAO WANAFUNZI 20

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akizungumuza na wanafunzi waislam waliofanya maandamano ya amani na kukusanyika viwanja vya Kidongo Chekundu Jijini Dar Es Salaam kupinga uongozi wa shule ya Sekondari ya Ndanda kuwafukuza wanafunzi wa kislam 20 waliokua wakisoma katika shule hiyo.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akiwasili kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu kuzungumuza na wanafunzi wa Kiislam waliokua wameandamana Dar Es Salaam kupinga kufukuzwa kwa Wanafunzi wenzao 20 katika shule ya Sekondari ya Ndanda.
 Rais wa wanafunzi wa Kiislam, Jafari Mneto akizungumuza kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu Jijini Dar Es Salaam baada ya wanafunzi wa Kiislam kufanya maandamano ya amani kupinga kufukuzwa kwa wanafunzi wa kiislam katika shule ya Sekondari ya Ndanda.
 Wanafunzi wa Kiislam wakiwa wamekusanyika kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu baada ya kufanya maandamano ya amani Jijini Dar Es Salaam kupinga kufukuzwa kwa wanafuzi 20 wa Kiislam katika shule ya Sekondari ya Ndanda.
 Polisi wakiwa wamekaa kwa tahadhali katika maandamano hayo ya amani yaliyofanywa na wanafunzi wa Kiislam Jijini Dar Es Salaam kupinga kufukuzwa kwa wanafunzi 20 wa kiislam katika shule ya sekondari ya Ndanda,
 Juu na chini ni Wanafunzi wa Kiislam waliofanya maandamano ya amani Jijini Dar Es Salaam leo kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu wakiwa wameshika mabango kupinga kufukuzwa kwa wanafunzi wa Kiislam 20 katika shule ya Sekondari ya Ndanda
Picha kwa hisani ya Michuzi

No comments: