ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 10, 2012

WASAIDIE WATOTO HAWA


Na Mwandishi wetu
KATIKA gazeti la Uwazi, toleo la wiki iliyopita lilitoa habari za mtoto Mustafa Ally, 12, (pichani), mkazi wa Mtoni Mtongani, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam anayewauguza wadogo zake mapacha wenye umri wa miezi nane.
Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.
Watoto hao mapacha wanaumwa na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mama yao aliyekuwa akiwauguza aliugua ghafla na kupewa matibabu na kwa sasa yupo hoi nyumbani kwake, hivyo Mustafa kuchukua mzigo huo wa kuwauguza.
Matatizo yanayoikabili familia hiyo ni pamoja na ukosefu wa chakula, nguo za kawaida na za shule, fedha za matumizi, maziwa ya unga ya watoto na kodi ya nyumba.
Gazeti hili kwa niaba ya familia hiyo linatoa shukrani kwa watu mbalimbali waliompatia msaada wa maziwa, sabuni, sukari, nguo na fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000.
Bado msaada unakaribishwa kwa watoto hawa. Aliyeguswa na kilio cha mtoto Mustafa afanye mawasiliano na Afisa Ustawi wa Jamii Muhimbili, Erika Ishengoma kwa simu 0714 220 038 au mwandishi wetu kwa namba 0713 454 656 au afike Muhimbili wodi ya watoto, Makuti B atakutana nao ana kwa ana.

6 comments:

Anonymous said...

Kumradhi jamani sikuhizi bongo hata watoto wasiojiweza wanavaa dippers ?

Anonymous said...

mdau hapo juu umeambiwa watoto wako muhimbili hosp kwa hiyo nina uakika kuna wasamalia wema ambao wanapitisha misaada mbalimbali kwenye hiyo wodi ya watoto.cha muhimu ni kusaidia hiyo familia

Anonymous said...

wewe ulietoa comment ya kwanza huna aibu nenda kajifukie

upumba ndo umekujaa kichwani kwa kuandika ulichoandika

masikini ni wewe na huko ulaya sijui wapi umasikini umekujaa wewe

unatia aibu

Anonymous said...

Nyinyi mlionijubu nyote hamna busara. Nimeanza na kuomba msamaa tena kinyenyekeve. Comment yangu imeanza na KUMRADHI.sababu enzi nilizoondoka Mimi Bongo ilikuwa matajiri tu! Ndo wanavaa Dippers.
Mlitakiwa mnijibu Yes zipo zinatengenezwa na Bakhresa au mengi au zimetolewa muhimbili nyinnyi mna condem tu! You all need some chill pills.

Anonymous said...

Mdau wa pili thank you nimekupata nilidhani zinauzwa bwelele sababu Zao la Pamba au Sufi Tanzania limejaa kumbe wamepewa msaada duh! Mpaka Leo Tanzania haitengenezi Dippers za Watoto? Na Pamba tunayo.kazi kweli kweli.even after 50 yrs of independence? Ok Asante kunijibu.Mimi ndo nilie uliza swali la kwanza

Anonymous said...

Jamani huyo mama hana ndugu au ndugu wa mume wa kuweza kuwatunza hao watoto badala ya huyo kaka yao Mustafa wa miaka 12. Hivi si kuna Ustawi wa Jamii?