Kushoto ni Mh. Balozi, Ombeni Sefue akiwaaga wanajumuiya wa New York kwenye Hafla fupi iliyofanyika Mjini humo Alhamisi February 16, 2012.
Mh. Balozi Ombeni Sefue (kati mwenye suti anaesalimia) akisalimiana na Watanzania wa New York mara alipoingia kwenye Hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika mjini humo, kushoto ni Hajji Khamisi, mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania, New York.
Shaban Mseba kati ya viongozi wa Jumuiya akimaribis ha Mh Balozi na huku akitoa shukran zake, kulia kwake ni mwenyekiti wake Hajji Khamis akimsikili za kwa makini.
Mwenyekiti akimkaribisha Mh Balozi.
Zawadi kwa Mh. Sefue ya kuonyesha shukrani na kazi nzuri aliyoifanya ambayo haitasahaulika kutoka kwa Wanajumuiya wa New York.
Mh. Balozi, Ombeni Sefue akiongea machache ya kuwaaga Wanajumuiya New York na kuwahusia mshikamano na kushirikiana ndio nguzo kuu ya kuendeleza umoja wao.
kutoka shoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Hajji Khamisi, Mh. Balozi Ombeni Sefue, Mh. Balozi wa kudumu wa Somalia Umoja wa Mataifa, Dr. Elmi Ahmed Dualeh wakipata picha ya pamoja.
Mh. Balozi Ombeni Sefue ( wapili toka shoto) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya na Watanzania wa New York waliofika kwenye Hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Alhamisi February 16, 2012 Mjini humo.
Kutoka kushoto ni Balozi wa kudumu wa Somalia Umoja wa Mataifa New York, Dr Elmi Ahmed Dualeh, Mama Sefue, Mh. Balozi Ombeni Sefue na Mke wa Balozi wa Somalia Mama Duealeh, wakipiga picha ya pamoja kwenye Hafla fupi ya kumuaga Balozi Sefue iliyofanyikia New York, Alhamisi February 16, 2012.
(Picha kwa hisani ya muakilishi wa VIJIMAMBO BLOG NYC,Ebra NY)

No comments:
Post a Comment