Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Azam FC, Stewart Hall amekanusha taarifa kuwa kiungo wa timu hiyo, Mrisho Ngassa alifuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa aliyoyafanya mwaka jana nchini Marekani katika klabu ya Seattle Sounders.
Ngassa ambaye alipata nafasi ya kucheza dhidi ya Manchester United alipokuwa kwenye majaribio hayo, ilielezwa kuwa amefanya vizuri na angeitwa kufanya mazungumzo juu ya kusajiliwa mwishoni mwa msimu uliopita.Akizungumza na Championi Ijumaa, Stewart alisema wenyeji wa Ngassa katika majaribio hayo walifurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na winga huyo lakini hakuwa na ubora wa kucheza katika Ligi Kuu ya Marekani.
“Nilishangazwa na taarifa zilizokuwa zimeenea mara baada ya Ngassa kumaliza majaribio yake, hakufuzu, kilichotokea ni kwamba walimsifia kwa kiwango alichoonyesha katika mazoezi waliyompa,” alisema Stewart na kuongeza:
“Ukiangalia Ngassa anatoka katika ligi yenye ubora mdogo ukilinganisha na ile ya Marekani, jambo ambalo lingemlazimu kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufikia kiwango cha kucheza ligi hiyo.
“Nadhani hilo pia ndilo lililosababisha acheze chini ya kiwango katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Bara kwa kuwa bado alikuwa na ndoto za kwenda kucheza soka la kulipwa nje.”
Viongozi wa Azam FC, waliwahi kusema Ngassa alifuzu baada ya kucheza katika mechi ya kirafiki ya Seattle Sounders dhidi ya Manchester United ya England.

Chanzo:GPL
1 comment:
C'mon guys...yaani kwa akili zenu mnataka kuniambia kuwa Ngassa mchezaji? Kwa mpira upi ama kipaji kipi? Si alikuja hapa Marekani na mkaona alivyoboronga. Jamaa kukimbia anajuwa sana tena sana tu ila hana kipaji hata kidogo. Huyu ni kama vile Hasheem Thabeet tu tofauti yao ni kwamba Hasheem alikuwa na potential Ngassa hajawahi na hana tu.
Post a Comment