Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mh. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa pamoja na Waziri kivuli Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekia Wenje wakiwa kwenye mkutano na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Ijumaa February 3, 2012 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Kaimu Balozi Mh. Lily Munanka (kulia) akiwa na Maafisa Ubalozi kutoka kushoto, Suleiman Saleh na Abbas Missana katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Maafisa, Brigedia jenerali Maganga, Mama Kiju na Suleiman Saleh wakiwa katika mkutano huo.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe (CHADEMA).
Kushoto na Dr, Switebert Mkama akiwa na Afisa Mindi Kasiga.
Kushoto ni Afisa Edward Masanja akiwa na Afisa Agnes Lusinde.
Kutoka kushoto ni Afisa Mindi Kasiga, Afisa Suleiman Saleh, Dr Switebert Mkama, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe, Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu, Afisa Kiju, Kaimu Balozi, Mh. Lily Munanka, Afisa Abbas Missana, Afisa Agnes Lusinde, Afisa Edward Masanja na Brigedia Jenerali Maganga wakiwa katika picha ya pamoja.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akisaini kitabu cha wageni.
Kiongozi kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe akisani kitabu cha wageni.
Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamtaifa, Mh. Ezekia Wenji akitia saini kitabu cha wageni.
Kutoka kushoto ni Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe, Kaimu Balozi, Mh. Lily Munanka, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyialandu na Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje wakipata picha ya pamoja.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyialandu na Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje wakiangalia Khanga ya Uhuru.
Kutoka kushoto ni Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje, Kaimu Balozi, Mh. Lily Munanka, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyialandu, Afisa Mindi Kasiga na Kiongozi wa kmbi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe wakiiangalia Khanga ya Uhuru.
Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje, Kaimu Balozi, Mh. Lily Munanka, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyialandu, Afisa Mindi Kasiga na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe wakiwa nje ya jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu leo alitembelea Ubalozi wa Tanzania hapa Marekani na kufanya mazungumzo na Maofisa wa Ubalozi.
Mh. Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Singida Vijijini aliongozana na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe na Waziri Kivuli wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Ezekia Wenje.Kwenye mazungumzo hayo Mh. Nyalandu alisisitiza umuhimu wa kukuza spirit of enterprise kama Taifa ili Watanzania wa nyumbani na ughaibuni waweze kufanya kazi kwa kibidii na kupinga dhana potofu kwamba Watanzani sio wachapa kazi.
Pia Mh. Waziri Nyalandu aliongelea umuhimu wa kukuza na kuendeleza demokrasia Nchini ili kusukuma maendelo ya Taifa letu.
Kwa upande mwengine kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe, yeye alielezea ukomavu wa demokrasia Nchini na kusifu kiwango tulichofikia sasa, alisema miaka ya nyuma asingedhani kuwa angeweza kufika Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC. na kufanya mkutano na Maofisa Ubalozi na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani.
Kaimu Balozi, Mh. Lilian Munanka aliwashukuru viongozi hao kwa kutembelea Ubalozi na kuhimiza ushirikiano pindi wanapotembelea Marekani hususani Makao Makuu hapa Washington.
Mh. Waziri Nyalando, Mh. Mbowe na Mh. Wenje wako Marekani kuhudhuria kongamano la kila mwaka la sala.
No comments:
Post a Comment