ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 22, 2012

Milwaukee yatangaza siku ya Tanzania

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. MwanaidiSinare Maajar akiongea na Wakuu wa Biashara na Makampuni ya Jimbo la Wisconsin kuhusu Tanzania na fursa za uwekezaji nchini Tanzania kwenye
mkutano ulioandaliwa na World Trade Centre Wisconsin kwa kushirikiana na AO Smith tarehe 20.02.2011
Balozi Maajar akimsikiliza mwalimu wa Chuo cha MATCakionyesha mitambo ya kujifunzia na kuelezea jinsi wanafunzi wa chuo
hicho wanavyotumia teknolojia kujifunza kwa vitendo mitaala ya ufundi
wa nishati ya umeme tarehe 20.02.2012
Balozi Maajar akiwa kwenye studio ya radio ya WUWM(Milwaukee Public Radio) akizungumzia madhumuni ya ziara yake Jimboni
Wisconsin kwenye kipindi mashuhuri cha Lake Effect kinachorushwa na
mtangazaji Mitch Teich jijini Milwaukee tarehe 20.02.2012
Listen to full Lake Effect Radio Interview at
Juu na chini ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. MwanaidiMaajar akiwa na Meya wa Mji wa Milwaukee Mhe. Tom Barrett wakionyesha
bango lenye hati ya kuitambua siku ya tarehe 20.02.2012 kama siku ya
Tanzania mjini Milwaukee.
Balozi wa Tanzania nchini marekani Mhe. MwanaidiSinare Maajar akipewa zawadi na Makamu wa Rais wa kampuni ya A. O. Smith Corporation Bw. Steve Rettler mara baada ya kuzungumza na wawakilishi wa makampuni takriban thelathini kutoka miji mbalimbali ya Wisconsin wenye nia ya kufanya biashara na Tanzania tarehe 20.02.2012
Juu na chu=ini ni Balozi Maajar akiwa kwenye picha ya pamoja nabaadhi ya Watazania waishio kwenye mji wa Milwaukee, Jimbo la Wisconsin waliofika hotelini kwake kumpokea mara baada ya kuwasili
mjini hapo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 19-22.02.2012
Balozi Maajar (katikati) kwenye picha ya pamoja uongozi wa Chuo cha ufundi cha Milwaukee Area Technical College baada ya kumaliza mazungumzo ya awali kuhusu kuanzisha ushirikiano kati ya chuo hicho na mojawapo ya chuo cha ufundi cha Tanzania. Kushoto kwa balozi ni muasisi wa ushirikiano wa miji ya Milwaukee na Morogoro, Ryan Skyfe na kulia kwa balozi ni Makamu wa Rais wa Chuo hicho Bibi Vicki Martin akifuatiwa na Rais wa Chuo hicho (mwenye tai) Bw. Michael Burke tarehe 20.02.2012.

(Habari na Picha kwa hisani ya Mindi Kasiga)

Meya wa Milwaukee atangaza siku ya Tanzania, Mjini Milwaukee Wisconsin

Meya wa Milwaukee kwenye Jimbo la Wisconsin amemtunukia Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar hati ya kuitambua siku ya tarehe 20.02.2012 kama siku ya Tanzania mjini Milwaukee.
Mayor Thomas Barrett ametangaza siku hiyo ofisini kwake leo (jana) kama sehemu ya kuipongeza Tanzania kwa kutimiza miaka 50 ya uhuru na kuendeleza ushirikiano baina ya miji dada (sister cities) ya Milwaukee nchini Marekani na Morogoro nchini Tanzania.
Katika hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, Meya Barrett na Balozi Maaajar walikubaliana kuendeleaza ushirikiano baina ya miji hii miwili, ulioanzishwa mwaka 2006, na pia kushawishi wawekezaji na wafanya biashara wa ukanda huu wa Marekani kuwekeza Tanzania.

Balozi Maajar yuko Jimboni Wisconsin kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyoandaliwa na muasisi wa ushirikiano wa miji ya Milwaukee na Morogoro Bw. Ryan Skyfe, ambapo anakutana na taasisi za elimu, biashara na wawekezaji mbalimbali kwa nia ya kuangalia maeneo ya ushirikiano wenye tija ili kuleta maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Baadhi ya taasisi alizofanya nao mazungumzo ni Milwaukee Area Technical College walioko kwenye Jimbo la Wisconsin mjini Milwaukee ambao wamekubali kushirikiana na mojawapo ya chuo cha Tanzania na kutoa elimu inayolingana na mitaala ya chuo hicho ambacho kinaongoza kwenye Jimbo hili kwa kutoa elimu ya vitendo kwenye sekta ya nishati ya umeme inayowasaidia Wamerekani kupata ajira.
Wengine ni Phoenix Financial & Investment Services walioko Jimbo la Illinois mjini Chicago na Helios Solar Works walioko Jimbo la Wisconsin Mjini Milwaukee. Balozi Maajar pia alipata fursa ya kutoa mada kwenye mkutano uliovutia wakuu wa biashara na wawakilishi wa makampuni wapatao thelathini kutoka kwenye Jimbo la Wisconsin wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Aidha Balozi Maajar alitumia fursa hiyo kuirajamu Tanzania na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo baina ya serikali za nchi hizi mbili kwa wananchi wake kuwekeza na kuendeleza ushirikiano kwa manufaa yao.
Kila mwaka Balozi wa Tanzania nchini Marekani  huandaa ziara mahsusi kwa ajili ya maafisa wakuu wa makampuni ya  kimarekani kutalii Tanzania na kuangalia fursa za uwekezaji na biashara nchini Tanzania. Ziara hiyo ambayo inachanganya biashara na utalii (business and leisure) imekuwa mashuhuri sana miongoni mwa wafanyabiashara wa Kimarekani ambapo mwaka huu inatarajiwa kufanyika tarehe 22 Juni – 02 Julai, 2012.
Balozi Maajar kesho tarehe 21.02.2012 anatarajia kukutana na Gavana wa Jimbo la Wisconsin Mjini Madison na baadae kuendelea na ziara yake kwenye miji ya La Farge na La Crosse Jimboni Wisconsin kabla ya kurejea mjini Washington, jimbo la District of Columbia.

Imeandikwa na Mindi Kasiga,
Wisconsin, Marekani.
20.02.2012

No comments: