WANAFUNZI wa shule ya msingi ya Rauya, Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, wako hatarini kukosa chakula cha mchana, baada ya baadhi ya wazazi kushindwa kuchangia ununuzi wa sufuria jipya baada ya lililokuwa likitumika kutoboka.
Akizungumza katika kikao cha wazazi kilichofanyika juzi shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Uforo Minja, alisema wazazi hao waliombwa kuchangia sufuria mwaka jana, lakini idadi ya waliolipa haifiki hata robo yao.
Minja alisema kila mzazi alitakiwa kulipa Sh 1,500 ili kupata sufuria lenye ukubwa wa kuchukua madebe sita ya maji, ili kutosheleza chakula cha wanafunzi wote, lakini mpaka sasa wameshindwa kununua kutokana na baadhi yao kutochanga.
Waliohudhuria kikao hicho, walitaka wazazi wa wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana na kuondoka na madeni, majina yao yasomwe katika makanisa wanakoabudu ili wafuatwe wayalipe.
Mmoja wa wazazi hao, Monica Lyamuya, alisema kwa kuwa wazazi hao waliotakiwa kulipa mwaka jana na mpaka sasa hawajalipa, walipe deni hilo pamoja na faini ambayo badala ya kulipa Sh 1,500 walipe Sh 2,000 ili kuwapa funzo wakati mwingine walipe kwa wakati, kwani dawa ya deni ni kulipa na si kulikimbia.
Lyamuya alisema mpishi wa shule hiyo amekuwa akipata shida wakati wa kupika na kumlazimu kutanguliza unga kwenye sufuria ili kuzuia kuvuja, kwa sababu wazazi wachache wanakwepa majukumu yao huku Serikali ikisisitiza wanafunzi kupata chakula cha mchana shuleni katika kukabiliana na utoro.
Wazazi wengine walipendekeza wenzao ambao hawajalipa wakamatwe na mgambo na kulipa faini na wengine wakapendekeza wac hukuliwe mbuzi wao na wauzwe mnadani ili kufidia wanachodaiwa.
Aidha, wengine walitaka uongozi wa kata ushirikishwe kufuatilia wadaiwa sugu, baada ya madai kuwa uongozi wa kijiji hicho umekuwa ukiwapa ahadi hewa za kufuatilia watuhumiwa hao.

1 comment:
jamani kwa kweli ni aibu kusikia kuwa wanafunzi wanakosa lunch sababu sufuria imetoboka. Kwani sufuria lina cost kiasi gani mpaka shule nzima ishindwe kuaford? basi wangewaomba hata mbunge mmoja atoe hiyo hela kuwaweza kuwasaidia. Jamani kwa hii posho mpya ya wabunge ya $330000, kwa nini wasitoe kiasi cha hiyo fedha na kusaidia. maana tunawaona bungeni wamelala na hawafanyi lolote still wanalipwa.
Post a Comment