Imani Makongoro
KATIKA hali ambayo ni nadra kusikika, mabingwa wa soka nchini Yanga wamesema wanawaombea wapinzani wao Simba washinde katika mechi ya marudiano dhidi ya timu ya Kiyovu ya Rwanda, kwa vile wanaamini ushindi kwao ni sifa kwa Watanzania wote na siyo Simba peke yao.
KATIKA hali ambayo ni nadra kusikika, mabingwa wa soka nchini Yanga wamesema wanawaombea wapinzani wao Simba washinde katika mechi ya marudiano dhidi ya timu ya Kiyovu ya Rwanda, kwa vile wanaamini ushindi kwao ni sifa kwa Watanzania wote na siyo Simba peke yao.
Simba inatarajia kurudiana na Kiyovu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Machi 2 au 3, huku Wekundu hao wa Msimbazi wakijivunia sare ya ugenini ya bao 1-1 Jumamosi iliyopita katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Yanga wanaamini kuwa Simba wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano itakayofanyika jijini Dar es Salaam, wakati wao wakienda Misri kwa kurudiana na Zamalek baada ya sare ya 1-1 wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Wakati Yanga ikitoa kauli hiyo, Jumamosi iliyopita ilishuhudia mashabiki wa Simba wakiwashangilia wapinzani wao Zamalek kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Celestin Mwesigwa alisema klabu yao haioni sababu ya kutoiombea Simba mazuri pale linapokuja suala la kitaifa.
"Maombi yetu ni timu zote za Tanzania zipite, hatuwezi kuiombea Simba itolewe kutokana na upinzani uliopo baina yetu na wao. Wao (Simba) na sisi tuko ndani ya Tanzania. Ni lazima tuombeane ili tuleta sifa Tanzania," alisema.
Akiongelea kitendo cha mashabiki wa timu yake kununua jezi za Kiyovu kama walivyofanya wale wa Simba katika mechi yao dhidi ya Zamalek, Mwesigwa alisema wao kama viongozi wa Yanga hawawezi kuwazuia mashabiki kununua na kuvaa jezi hizo katika mechi ya marudiano ya Simba na Kiyovu.
"Kila shabiki ana uhuru wa kiushangilia timu anayoipenda hivyo mwenye maamuzi ya kuvaa jezi ya Zambarau na Kijivu katika mechi ya Kiyovu na Simba ni shabiki mwenyewe sisi hatuwezi kumzuia," alisema.
Kauli kama hiyo pia iliwahi kutolewa na Mwenyekiti wa Simba Aden Rage kufuatia mashabiki wa timu yake kununua jezi za Zamalek kwa lengo la kuwaunga mkono kwenye mechi dhidi ya Yanga.
Alikaririwa akisema; "Simba haina uwezo wa kuwazuia mashabiki wake kushangilia timu nyingine wanayoipenda. Kwa maana hiyo, kama wataishangilia Zamalek, hilo siyo agizo letu ila uamuzi wao binafsi."
Kuhusu maandalizi kwa ajili ya mechi ya marudiano, Mwesigwa wanajipanga vizuri ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ya marudiano ugenini.
"Tulijiandaa katika mechi zote mbili lakini bahati mbaya mechi ya kwanza tukiwa nyumbani timu yetu ilitoka sare ya 1-1. Tunajiandaa kurekebisha makosa yaliyotokea na mwalim ameshaanza kazi hiyo," alisema.
No comments:
Post a Comment