ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 31, 2012

THE 2ND ANNIVERSARY OF VIJIMAMBO MARCH 31, 2012

TAFADHALI TUNZINGATIE MUDA MHE. BALOZI ATAINGIA UKUMBINI SAA 2 (8 PM) NAWAOMBA WATANZANIA WENZAGU TUENDE NA MUDA ILI KWA PAMOJA TUMKARIBISHE MGENI WETU MHE. MWANAIDI SINARE MAAJAR, SHEREHE ZA USIKU ZINAANZA SAA 1 JUU YA ALAMA (7.00 PM)
MABADILIKO YA RATIBA
Kutokana na Timu za Serengeti Boyz ya Houston (TX) na Kili Stars ya North Carolina kushindwa kufika kwa sababu zilizokua nje ya uwezo wao 
Sasa Sherehe zitaanzia saa 4:00 Asubuhi (10:00am) Mpaka saa 12:00 jioni (6:00 pm) kwa mechi za soccer kugombea Kombe la VIJIMAMBO timu zitakazoshiriki ni:
Burundi kutoka Arizona
Tanzanite kutoka Atlanta, GA
DC Nyarugusu Watanzania Kutoka DC.
Vitambi FC Wakenya Kutoka DC
Malawi kutoka DC
na Stars United.

Mechi zitachezewa
8000 Walker Mill Rd,
Capitol Heights, MD 20747

Na kufuatiwa na Sherehe ya usiku zitakazoanza saa 1:00 jioni (7:00 pm) Tafadhali naomba uzingatie muda.
RADIO MBAO ITARUSHA PARTY YA VIJIMAMBO LIVE

Napenda kutoka shukurani kwa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Wadhamini waliojitokeza na shukurani za pekee ziwaendee Wadau wa VIJIMAMBO waliojitokeza na kujitolea kuleta chakula, vinywaji  na kupamba ukumbi ili sote kwa pamoja tufanikishe sherehe hizi kwani pamoja tunaweza.

PARTY YA USIKU NI KWA WATU WAZIMA TU

DRESS TO IMPRESS

HALI YA HEWA

6I-45 kutakua na shower asubuhi mechi za mpira wa miguu zitakuwepo kama kawaida zitachezewa kwenye turf field tujitahidi kuwahi na hakutakua na BBQ
 Asante
-------------------------------------------------------------------
RATIBA YA USIKU PARTY SHEREHE ZA MIAKA 2 YA VIJIMAMBO BLOG
TAREHE 03/31/2012
THE MIRAGE HALL
1401 UNIVERSITY BLVD
HYATTSVILLE MD 20783
MUDA
SHUGHULI
WAHUSIKA

1:00 – 2:00 USIKU

Wageni mbalimbali kuwasili kwenye ukumbi wa Mirage Hall


Kamati ya Maandalizi

2:05 – 2:20 USIKU

Kuwasili kwa Mgeni Rasmi na Kukaguwa mabanda ya wajasiriamali na wafanyabiashara wadogowadogo


Mhe Balozi Mwanaidi Sinare Maajar




2:20 – 2:25 USIKU

Wimbo wa Taifa

Linah 


2:30 – 2:45 USIKU


Lady in Red Fashion Show

Asia Idarous

2:50 – 3:50 USIKU


Chakula 


Kamati ya Maandalizi

3:55 – 4:00 USIKU

Bongo Flava


Bongo Flava Artist

4:05 – 4:15 USIKU

Mmiliki wa Vijimambo Blog Kumkaribisha Mhe Balozi Mwanaidi Sinare Maajar 

Lucas Mukami


4:20 – 4:30 USIKU 

Balozi Kukabidhi Kikombe Kwa Mabingwa
Wa Mashindano ya Mpira

Mhe Balozi Mwanaidi Sinare Maajar



4:35 - 4:45 USIKU



Mh. Balozi Maajar kuzungumza machache

Mhe Balozi Mwanaidi Sinare Maajar



4 :50 - USIKU ni  MUZIKI na Dj Kay akishirikiana na Dj Luke


MSHEREHESHAJI NI SUNDAY SHOMARI

No comments: