ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 20, 2012

AFYA YA MZEE GURUMO YAZIDI KUIMARIKA

Msanii Mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo akiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam jana akipimwa mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali hiyo, Suraiya Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita.
(Picha na www.burudan.blogspot.com)
---
MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya  Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super'D' alisema Afya ya  Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina kujua kila kitu kinachomsumbua  katika mwili wake.

"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivi karibuni"alisema Super D.

Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea mwanamuziki huyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wiki hii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege mkoa wa Pwani, Ijumaa
watapiga katika viwanja vya Leaders Club, Jumamosi watakuwa katika viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wikiendi katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni alisema Super D.

No comments: