ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 28, 2012

HOUSTON: Hati za Kusafiria(Passport)

Napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha wanajumuia ya Houston, Texas na vitongoji vyake, pamoja na Watanzania kutoka jumuia nyingine hapa Marekani ambao watakuwepo Houston tarehe 11, mwezi wa tano(05), 2012, kwa wenyekuhitaji kubadilisha au kuchukua Hati mpya za kusafiria(passport), kwamba maofisa wa Ubalozi wetu wa Tanzania kutoka Washington DC, watakuwepo Houston kwaajili ya zoezi hili la utoaji wa vibali vya kusafiria, asubuhi ya tarehe 11, 2012. Usiache nafasi hii ikupite, mfahamishe ndugu, rafiki na jamaa. Viongozi wa jumuia mbalimbali tunaomba mtusaidie kuongeza ufanisi wa usambazaji wa habari hii. Anuani ya sehemu ya zoezi hili itatolewa, au wasiliana na viongozi wa jumuia ya Houston,
Erasto Mvungi: Mweka hazina, 832-486-0678
Lilian Kasapira: Makamu Katibu, 832-646-3087
Leyla Kikuzi: Katibu, 713-382-7135
Ahsanteni,

Novastus Simba,
Mwenyekiti wa jumuia ya Watanzania Houston,
Simu:   832-208-8344

No comments: