Advertisements

Sunday, March 18, 2012

Music Academy wakamua Dar Live

 Paul Mwanja mpiga drum wa academy akiwa mzigoni.
 Paul Mwanja mpiga drum wa academy akiwa mzigoni.
Wana Academia wakiimba wimbo wao mpya unaoitwa linda. 
 mwalimu(Hamza Kalala) akiwapa tafu kupiga gitaa la solo ndani ya dar live
Wana Academia wakiimba wimbo wao mpya unaoitwa linda. 
salam,
 
Baada ya kufanikisha uundwaji wa Music Academy Tanzania chini ya usimamizi wa ASET na URBAN PULSE CREATIVE kwa mara ya kwanza wana academia walipata fursa ya kutumbuiza live stejini katika ukumbi mpya wa kisasa Dar Live uliopo mbagala siku ya  jumamosi tarehe 17.3.2012
 
Hii ilikuwa ni mojawapo ya hatua waliopiga kuonyesha vipaji vyao na kuwajengea uzoefu kutumbuiza mbele za maelfu ya mashabiki waliojitokeza kupata burudani.
 
Music Academy inaendelea kutoa mafunzo na pia kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yataendela kufanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
 
Asanteni,
 
ASET  na URBAN PULSE CREATIVE

2 comments:

Anonymous said...

Safi sana tuendeleze muziki wetu na hii ya kukopi na ku paste kisha kuibatiza kuiita yetu.

Anonymous said...

Siku huo mwimbo ukiingia YouTube tuwekee hapa DJ Luke . Umetungwa special kwa Mlembwende sister Linda express au Linda yupi? Au unazungumzia nini?