waziri wa nishati na madini Adamu Kigoma Malima
NAIBU waziri wa nishati na madini Adamu Kigoma Malima ameibiwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 katika hotel ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro ambapo alikuwa amefikia kwa siku tatu.
Kwa mujibu wa mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoani hapa Hamis Seleman alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10.45 alfajiri katika hotel hiyo na kwamab uchunguzi wa awali ulibaini kuwa waziri huyo alikuwa amejipumzisha katika sebule ya chumba hicho na kwamba ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani kwake na kutoa taarifa kwa uongozi wa hotel hiyo.
Vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na Dola 4000 za Marekani, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, pete za silva 2 zenye thamani ya shilingi milioni 2, simu zenye thamani ya shilingi milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya shilingi 50,000, laptop 2 zenye thamani ya shilingi milioni 5.6, taperecorder na headphone milioni 1.
Mazingira ya wizi huo ni kuwa dirisha la chumba hicho ambalo ni la Alminium limevunjwa na kitu cha chuma na hivyo kusababisha mwizi huyo kuingia ndani na kuiba.Alisema kuwa nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo za mwizi pamoja na ndani ya chumba hicho jambo lililoashiria mwizi huyo kuingia hadi ndani hakuna mtu aliyekamatwa.
Al\kizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo na kuthibitisha kuibiwa vitu hivyo Malima alisema kwamba kinachomuuzunisha ni pete yake ya urithi aliopewa na marehemu baba yake pamoja na moja aliopewa na mkewe.
Alisema alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Morogoro kwajili ya kukagua miradi ya madini na kwamba baada ya kurudi alikaa katika sebule ya hotel hiyo akiangalia taarifa ya habari na kupitiwa na usingizi na kusinzia ambapo alipostuka 10.45 ndipo aligundua kuibiwa vitu hivyo.
Alisema kuwa bunduki na bastola yake havikuibiwa ingwa vitambulisho, pasipoti pamoja na kadi za benk pamoja na dokumenti zake za ofisi zimeibiwa.

2 comments:
watu wachukua madini na nishati zao 2
Hiyo ni inside job, lazima ni mfanyakazi wa hiyo hoteli. Wamejuaje chumba alichofikia? Mungu amemwepusha mengi what if angekuwa chumbani huyo mwizi angemmaliza maana waziri asingekubali achukue vitu vyake. Pole mheshimiwa but yote ni mipango ya mungu! At least you are alive.
Post a Comment