ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 23, 2012

Nizar Khalfan apewa masharti kuitwa Stars

Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Taifa Stars, Jan Poulsen amemtaka kiungo wa timu hiyo, Nizar Khalfan, kutafuta klabu ya kuichezea haraka kama anataka kuwemo kwenye kikosi cha Stars.
Nizar, ambaye awali alikuwa akikipiga katika klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada na baadaye kuhamia Philadelphia Union ya Marekani, hana timu kwa sasa kutokana na Union kuvunja naye mkataba kwa madai ya kushuka kiwango. Alirejea nchini hivi karibuni.

Poulsen ameliambia Championi Ijumaa kuwa amesikia taarifa kwamba kiungo huyo yupo nchini kutokana na kuachwa na klabu yake lakini akasisitiza kuwa anapaswa kuhakikisha anapata klabu haraka ili kuokoa nafasi yake katika kikosi cha Stars.
“Nimepata taarifa hizo ambazo binafsi zilinishtua lakini ninachoweza kumwambia yeye bado ni mchezaji mzuri na akihangaika ataweza kupata timu,” alisema Poulsen na kuongeza:
“Anapaswa kuhakikisha anatafuta timu haraka kwa kuwa moja ya sifa za mchezaji kuitwa kwenye timu ya taifa ni kuwa na timu ili kocha aweze kuangalia kiwango chake.” (Chanzo GPL)

No comments: