WATU sita wamepoteza uhai mkoani Tabora katika mazingira tofauti, wakiwemo wanne wanaoishi nyumba moja ambao wameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Watu hao wanne akiwemo mzee wa miaka 80 wameuawa katika kitongoji cha Shawilu Kijiji cha Mwambaha Kata ya Utwigu wilayani Nzega katika kile kinachoaminika ni imani za kishirikina.
Waliouawa ni Shija Saidi (43), Jane Kapela (80) Sanzu Kulwa (14) pamoja na Mgaka Charles (30).
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Antony Rutta akitoa taarifa ya vifo hivyo vilivyotokea jana na juzi kwa waandishi wa habari alisema wengine wawili wamekufa kwa kupigwa na radi walipokuwa nyumbani kwao.
Alisema watu hao walipigwa na radi hiyo wakijiandaa kupata mlo wa jioni katika kijiji cha Itonjanda, umbali wa kilometa 20 kutoka mjini Tabora.
Aliwataja waliokufa kuwa ni Kulwa Idd na Juma Issa, ambaye ni mtoto wa dada yake Juma.
Tangu Machi 17 mpaka Machi 25, watu zaidi ya watano waliuawa kwa mtindo huo wa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana kutokana na imani za kishirikina hali iliyozua wasiwasi kwa wananchi.

No comments:
Post a Comment