ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 26, 2012

Ulimi wako ni uchawi tosha kwenye mapenzi, jifunze kuutumia -2

 
Wiki iliyopita tulianza kujadili mada ya ulimi wako ni uchawi tosha kwenye mapenzi, jifunze kuutumia. Leo tunaendelea kuanzia pale tulipoishia.

SIJAWAHI KUKUSALITI (I have never cheated on you)
Jaribu kuanzisha mazungumzo kuhusu namna ambavyo unachukia usaliti. Mbele ya mazungumzo yako, mueleze kuwa unaridhika kuwa naye, kwa hiyo hujawahi kumsaliti hata mara moja.
Ni kawaida ya wivu kukua muda baada ya muda lakini wewe unayo nafasi ya kumfanya asiwe na chembe yoyote ya kukuhisi unamsaliti.


NINGEPOTEA BILA WEWE (I’d be lost without you)
Ni katika kumfanya ajione yeye ni taa ya maisha yako. Mueleze kuwa kama si yeye, ungeshapoteza muelekeo wa kimaisha. 
Kwa kawaida, mwanamke hataki tu kujua kuwa unampenda na kumtaka, ila unamhitaji kwa dhati, kwa hiyo ukimwambia ni yeye ndiye amekuweka kwenye mstari, atajiamini kuwa unamhitaji sana.

WEWE NI MCHESHI (You’re funny)
Daima tembea na kanuni hii. Wawili wanaopendana na kucheka pamoja ndiyo hudumu. Mpe uhuru akuchekeshe halafu uruhusu mbavu zako zivunjike kwa kicheko. Mwisho wa kicheko, gonganisha naye viganja halafu mwambie “wewe ni mcheshi sana mpenzi wangu.”

NAKUPENDA (I love you)
Ni neno la kawaida lakini kwa mwanamke huwa lina maana kubwa endapo litatamkwa na mtu anayempenda. Ni hatari kwa wanaume wengi wanapowazoea wapenzi wao, hushindwa kutamka neno hili lakini mwanamke hupenda kusikia akiambiwa hivyo.
Mwambie mpenzi wako jinsi unavyompenda, mthibitishie kuwa mapenzi yako kwake ni makubwa kupita kiasi.

VIPI KUHUSU WANAUME?
Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi. Hulaumu kwamba ni ngumu kubaini vitu ambavyo wanaume huhitaji kutoka kwa wanawake.
Wanadai kuwa wakati mwingine hujitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanawapa furaha lakini wanaume huwa hawana hata msisimko. 
Hapa chini, nimekuandalia vitu ambavyo wanaume huhitaji kwa wanawake wao. Moja kwa moja, mambo yakienda chanya huwa ni zaidi ya chombezo na hupagawa.

MAPENZI (Love)
Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao. Mara nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya upendo waliotoa kabla.
Wanapenda, kwa hiyo nao huhitaji kupendwa ili waone mambo yanakwenda sawa. Wanawake wengi huwa wanaficha hisia za kupenda, hili huwaumiza wenzi wao. Onesha mabadiliko, muoneshe jinsi unavyoridhishwa na upendo wake kisha mtamkie kwamba kwake umefika, halafu thibitisha hilo kwa vitendo.

MVUTO (Attractiveness) 
Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto. Hii inawezekana isiwe na maana kwa wanawake kwa kushindwa kutambua jinsi mvuto wao unavyoweza kuwa kibwagizo murua cha mapenzi.
Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu. Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote. Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.

UAMINIFU (Trustful)
Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100. Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe. Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao. Jiamini kisha uwe muaminifu. Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.

Itaendelea wiki ijayo.


www.globalpublishers.com

No comments: