MARAFIKI tunakutana tena katika safu yetu ya kuwekana sawa juu ya uhusiano wa kimapenzi. Nina imani kwamba mtakuwa wazima wa afya njema na mpo tayari kabisa kupokea darasa hili maridhawa.
Nazungumzia juu ya namna ya kutatua migogoro inayotokea katika mapenzi. Je, wewe unafanyaje? Kama mtakumbuka wiki iliyopita nilianza kwa kuelezea sababu za watu kukimbilia msaada kwa wengine kisha tukaona faida za kuwashirikisha watu wa karibu.
Kumbuka nilieleza kwamba, kwa namna yoyote ile, kuwashirikisha wazazi katika matatizo hasa ya kawaida ni kosa. Huwajengea wazazi kitu kibaya vichwani mwao na kuwa na wasiwasi na uhai wa ndoa/uhusiano wenu.
Ikiwa ni kweli, umeona tatizo ulilonalo huwezi kulimaliza mwenyewe mpaka uwashirikishe watu, basi iishie kwa marafiki wa karibu tu, tena wale ambao kwa namna moja ama nyingine wanaheshimiana sana na mwenzako.
Nilianza kwa kueleza faida za kuwashirikisha wengine katika migogoro, lakini kama ilivyo kawaida, siku zote kwenye faida kuna hasara zake, sasa leo tunakwenda kuona hasara za kuwashirikisha wengine katika mitafaruku, kabla ya kuona vipengele vingine muhimu. Twende tukaone.
HASARA ZA KUWASHIRIKISHA
Kuna hatari ya kuwashirikisha marafiki au ndugu wa karibu katika matatizo yenu hasa ya kawaida, ambayo katika hali ya kawaida mnaweza kuyamaliza hata kwa mazungumzo ya kawaida.
Zipo hasara nyingi sana, lakini hapa katika All About Love nimekuandalia zile muhimu zaidi tano. Unajua ni zipi? Karibu rafiki.

(i) Unaonekana hujiamini
Kitu kibaya kwa mhusika hasa yule anayepeleka matatizo kwa marafiki zake, ataonekana hajiamini. Hana maamuzi na hawezi kumaliza mambo yake mwenyewe.
Kwa namna yoyote ile ataonekana hana ‘kifua’ cha kudhibiti matatizo yake ya ndani ambayo hapa yanajulikana kama aibu ya mwenzake! Kukosea ni aibu marafiki. Kwa maana hiyo, kuwaeleza wengine namna mwenzako alivyokukosea ni kumuabisha!

(ii) Unapoteza kujiamini
Ukiachana na mhusika kuonekana hajiamini, hata yeye mwenyewe ataingia katika hatua ya mbali na kuanza kujiona kama hajiamini fulani hivi. Ni mazoea mabaya ambayo baadaye humlemaza na kujikuta kila kitu anataka kuwaambia wenzake.
Kama tabia hii ikiendelea kwa muda mrefu, kuna hatari ya kuwashirikisha marafiki zake hata mambo ya ndani kabisa ambayo hayapaswi kusikilizwa na mtu mwingine yeyote zaidi ya yeye mwenyewe na mwenzake.

(iii) Humilikisha amani na furaha ya penzi
Si jambo rahisi sana kugundulika mapema, lakini athari zake huanza kuonekana baadaye kabisa. Kama ni mgonjwa, daktari angeweza kusema: “Mgonjwa mmemchelewesha.”
Marafiki hili ni tatizo kubwa sana, maana kama utakuwa mtu wa kuwaeleza marafiki zako matatizo yenu ni wazi kwamba, amani ya uhusiano wako inakuwa imeshikiliwa nao. Ikitokea ugomvi kidogo tu, utawakimbilia ukiamini kwamba ndiyo wanaoweza kuwapatanisha.

(iv) Unaonesha udhaifu wa mwenzako
Jambo lingine kubwa hapa ni kwamba, kwa kuwashirikisha marafiki kuhusu migogoro yenu, ni wazi kwamba utaeleza alikufanyia nini ambacho kimekusukuma na kuhitaji usaidizi wao.
Kwa kiasi kikubwa ni kwamba, utakuwa unaonesha udhaifu wa mwenzako jambo ambalo si zuri kwa hakika. Ni rahisi pia mwenzako kudharauliwa hasa kama kosa lenyewe ni la ‘kitoto’ sana au ufahamu.

(v) Unawapa maadui nafasi
Kuna baadhi ya watu wana kasoro ya kutokuwa wasiri. Ni washauri wazuri. Unaweza kumweleza tatizo lenu na akalisuluhisha vizuri kabisa, lakini kwa bahati mbaya akawa na kasoro ya kibinadamu ya kutokuwa msiri.
Kutokana na hili, baada ya kumaliza usuluhishi, hujisahau na kuanza kuzungumza na wengine kuhusu mambo yenu. Hapo sasa utakuwa unawapa maadui nafasi ya kuingilia penzi lenu.
Ikiwa mmoja wa maadui zenu atanasa mgogoro wenu ni rahisi kuchochea zaidi ili ugomvi ulipuke zaidi, iwe furaha ya moyo wake. Wenyewe wanasema, ‘adui muombee njaa.’

MSAIDIE MWENZAKO
Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako. Kumbuka haishi na malaika, ni binadamu ambaye ana upungufu wake. Jenga uvumilivu na kuwa mtu wa kufundisha zaidi. Hata kama amekukosea jambo kubwa, jipe moyo.
Tulia, hasira zikiisha kaa chini na umweleze makosa yake. Bila shaka ataelewa na mtabaki salama katika uhusiano wenu. Nini nimeacha? Bila shaka nimemaliza na nimeeleweka vyema.
Hadi wiki ijayo katika mada nyingine kali, USIKOSE!

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na Who is Your Valentine? vilivyopo mitaani.
No comments:
Post a Comment