
KAMA kawaida tumekutana kwenye kona yetu ili kujuzana mambo mawili matatu yanayohusu mapenzi. Yangu hali namshukuru Rabuka, sijui kwako mwenzangu lakini kwa uwezo wake Maanani, nina imani u mzima buheri wa afya.
Gharama katika mapenzi zinatokana
na nini?
na nini?
Tumeona watu wengi wakishutumiana mmoja kuendekeza starehe au kupenda vitu vya gharama wakati akijua uwezo wa mwenzake haulingani na mahitaji anayoyataka.
Tuangalie madhara ambayo tunalaumu na kuona kama tunaonewa kumbe tatizo tunaweza kuwa sisi mwenyewe, huenda tulifanya bila kujua madhara yake ya mbeleni, halafu kesho na keshokutwa sisi ndiyo tunakuwa wa kwanza kulaumu.
Siku zote mwanaume kumpata mwanamke huwa na njia nyingi kwa kila mmoja kutumia uwezo wake, wapo wanaotumia chambo cha fedha ambacho huwa rahisi kumnasa mwanamke.
Wapo pia wataalam wa kupiga domo, hata mwanamke awe mgumu kiasi gani lakini akikubali kumsikiliza ajue amekwenda na maji.
Wapo ambao hufanya mapenzi yao kwa matangazo, kabla ya kumpata mwanamke huonyesha makeke ya kuvaa vizuri na kujionyesha wana fedha ili tu kuwanasa warembo.
Kwa vile katika maisha kila mwanadamu ana tabia zake, basi mwanamke naye ana mitego yake inayomnasa.
Aliyetumia domo akifanikiwa kuteka hisia za mwanamke kwa vile alipendwa kwa maneno matamu yasiyo na gharama, naye hatatumia gharama kubwa kuendesha uhusiano wao.
Aliyetumia domo akifanikiwa kuteka hisia za mwanamke kwa vile alipendwa kwa maneno matamu yasiyo na gharama, naye hatatumia gharama kubwa kuendesha uhusiano wao.
Aliyempata mwanamke kwa njia ya matangazo anakuwa na wakati mgumu wa kuhakikisha anafanya yale aliyoyafanya kabla ya kumpata mwenza wake, ili tu aendelee kupendwa.
Siku zote mwanzo wa hesabu huwa moja, bila kutarajia mnajikuta mkivuka mipaka na kuwa mke na mume. Nawe bado hutaki kuonekana ulizichanga ili kumpata, unaendeleza maisha ya kifahari kama vile kutembelea kumbi za starehe na pengine ambako ndiko ulikompatia mpenzi wako.
Inapotokea mwanaume umetumia gharama kubwa kumpata mwenza wako na Mungu kawajaalia mmekuwa mume na mke, hapo ndipo filamu linapokolea kwa kuwa umtalazimika kuishi maisha ya gharama ya juu ili umridhishe.
Siku hazilingani, unajikuta fedha unazozipata zinaishia katika chakula na starehe huku maendeleo yakikosekana.
Unapojaribu kumshawishi mwenzio mle dagaa na siku za mwisho wa wiki mpumzike nyumbani msitoke badala ya kutoka kama kawaida yenu, hakuelewi, hapo ndipo unapoanza kulalama juu ya mkeo kuwa wa gharama na kusahau wewe ndiye mhusika mkuu wa tatizo lile.
Jitahidi kuishi jinsi ulivyo kwa kutumia fedha zako ambazo hazitavuka kipato chako, lazima ujue mwana umleavyo ndivyo akuavyo.
Jiepushe kuishi maisha ya matangazo wakati uwezo wako ni mdogo. Aidha inapotokea mwanamke unapokuwa na rafiki yako wa kiume ukiona matumizi yake yanapitiliza kikomo mshauri ili hizo fedha ziwasaidie siku za mbeleni.
Jiepushe kuishi kwa starehe hasa ukiwa ndani ya ndoa, wewe ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuijenga nyumba yako au kuibomoa.
Tukutane tena wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment