Bongo Real FC
DC Nyarugusu SC
Timu za Bongo Real FC na DC Nyarugusu SC zitaungana mwaka huu na kuunda timu moja ya Tanzania na kuingia kwenye mashindano yanayojulikana kama 2012 DIASPORA WORLD CUP yanayoshirikisha Nchi mbali mbali zenye maskani hapa DMV.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza mapema mwezi wa April tarehe bado haijatajwa, Vijimambo ilipoongea na Jabir Jongo ambae yeye na Ally Bambino watakua wasimamizi wa timu kwenye mashindano hayo, ameomba wachezaji wote kuondoa tofauti zao za UDC Nyarugusu na Ubongo Real hii ni timu ya Tanzania na amesisitiza Mazoezi kuanza kesho Jumapili March 4, 2012 saa 10:30 jioni katika viwanja vya Meadowbrook park, alisisitiza wachezaji wajitokeze kwa wingi kwani ushindi huanzia kwenye mazoezi.
Jabir pia aliomba wachezaji ambao wapo mikoani wangependa kushiriki mashindano haya wawasilishe majina yao mapema.
No comments:
Post a Comment