TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH:-TIMU YA TAIFA YA NGUMI KUKABIDHIWA VIFAA VYA MAZOEZI NA
LAPF TAREHE 3/4/2012 SAA 4.00 KATIKA OFISI ZA LAPF MILLENIUM
TOWER KIJITONYAMA.
Awali ya yote shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) tunatoa shukrani za dhati kwa kwa shirika la LAPF kwa mara nyingine kukubali kuipatia timu ya Taifa ya ngumi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya maandalizi kushiriki mashindano ya kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Casablanca Morocco Aprili 27/2012 na hatimaye mashindano ya Olimpiki Julai 2012 London Uingereza.
Zoezi hilo litafanyika kesho tarehe 03/14/2012 kuanzia saa 4.00 asubuhi katika Ofisi za LAPF zilizopo jengo la Millennium Tower Kijitonyama.
Timu ya Taifa ya ngumi ipo kambini Kibaha katika shule ya Filbert Bayi ikiwa na jumla ya wachezaji kumi wa uzito wa kuanzia l/fly hadi super heavy ikiwa na jumla ya makocha watatu na dakitali mmoja.
Wachezaji na makocha waliopo kambini ni:-
- John Christian 49KG l/fly
- Abdalah Kassim 52 kg fly
- Emillian Patrick 56 kg bantam
- Denis Martin 60 kg l/weight
- Victor Njaiti 64 kg l/welter
- Seleman kidunda 69 kg welter
- Mohamed chibumbui 69 kg welter
- Mhina Moris 81 kg l/heavy
- Haruna Swanga 91kg heavy
- maximillan Patrick 91+ super heavy
- Edward Emanuel kocha
- David Yombayomba kocha
- Remy Ngabo kocha
- Joseph Magesa daktari
Wote mnakaribishwa kushuhudia tukio hilo kwa maendeleo ya mchezo wa ngumi
Makore Mashaga
Katibu Mkuu
No comments:
Post a Comment