ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 2, 2012

BigRight awakomalia vijana wadogo

Ibrahim kamwe`bigright` ambae ni local promoter wa ngumi ameamua kwa dhati kabisa kuwafundisha vijana wadogo mchezo huo. Ibrahim anasema “Mabondia wengi hapa nchini wanapigana ili mradi wanapigana hawana formula zozote,hawajui kujilinda pale wanapoelemewa,hushambulia kwa kubahatisha tu, pia hawajui sheria za mchezo wenyewe yote kutokana na kukurupukia mchezo ukubwani.
Bondia akicheza sparing kidogo anatafuta fight,na akipata fight moja au mbili basi huwezi kumkosoa kila kitu anajua yeye wakati ana mapungufu mengi na hajafikia kuitwa professional boxer.hivyo nimeamua kuwafundisha vijana wadogo ambao wanafundishika .kwani SAMAKI MKUNJE YUNGALI MMBICHI. Sio baadae tunailalamikia serikali.sisi tujitahidi then tuiamshe serikali itusaidie,sababu inatulazimu kujua kama serikali yetu imelala katika michezo mingine ambayo pia ndio inayoleta ushindi na sifa ulimwenguni.wenyewe wamelalia soka ambayo hawaiwezi ni kupeana matumaini tu.

Vijana wadogo wa timu ya ngumi ya Bigright  boxing wakiwa katika pozi la pamoja.na kiongozi wao Ibrahim bigright nyuma mwenye miwani na fulana nyeusi
Hawa ni vijana `A`walioanzaimprove kiasi cha kufanya show za boxing wapo katika muelekeo mzuri wa kuwa mabondia kamili na pengine kutuletea medals na tittles in a future.aghalabu sana kusikia nchini mwetu vijana umri huuu wanapewa kipaumble katika riadha, au boxing.
 Hawa vijana wa timu`B` ambao bado wanaendelea na mafundisho zaidi,ili kufikia muelekeo wa kibondia
Vijana wa bigright boxing ambao tumezoea kuwaona maukumbini  katika pozi wakiongozwa na Abdulbasit ibrahim-bigright jr ,  issa omar na herman shekivuli waliokaa
Bigright akimfua mmoja wa vijana wake issa omar.
Issa omar ni mmoja wa vijana wanaofanya vizuri keshacheza mara tisa na kushinda yote

No comments: