Kwanza napenda kuwashukuru wadau wa Vijimambo na Watanzania wote DMV waliopiga kura za maoni katika kinyang'anyiro cha Urais kati ya Mgombea Loveness Mamuya na Iddi Sandaly, kura za maoni zinaonyesha mpambano utakua mgumu, mshindi atashinda kwa kura chache.
Kura zilizopigwa ni 68, zilizoharibika kwa kutofuata masharti ni 29 na moja ilikua neutral, kura zilizokua sahihi ni 38 na Iddi Sandaly amemshinda Loveness Mamuya kwa Kura 4.
Hii haina maana kwamba Iddi Sandaly ndio ameshinda uchaguzi huu kwa sababu waliopiga kura za maoni si Watanzania wote na hapa DMV tupo Watazanania zaidi ya 1,000,
Vijimambo inawatakia kila la heri wagombea wote waliojitokeza kwenye kinyang'anyiro hiki na nawaomba Watanzania wenzangu DMV tunzingatie muda na tujitokeze kwa wingi ilikufanikisha zaoezi hili muhimu la kihistoria na la kujivunia kwa Jumuiya yetu iliyolegalega tangia 2007.
Mwenyezi Mungu aubariki uchaguzi huu uwe wa haki na amani, Mungu ibariki Jumuiya yetu, Mungu Ibariki DMV, Amina
Sasa hawa ndiyo wagombeaji katika nafasi kama zinavyo fuatana na majina yao,
A> Wagombeaji wa nafasi ya Uraisi:
1: IDDI SANDALY
2: LOVENESS EDWIN MAMUYA
B> MAKAMU WA RAIS:
1> RAYMOND ABRAHAM
C> Wagombeaji wa nafasi ya Katibu Mkuu:
1> YACOB KINYEMI
2> AMOSI CHEREANI
3> RHODA KASAMBA
D> Nafasi ya Mweka Hazina:
1> GENES MALASY
E> Wajumbe wa Bodi:
1> ELISERENA NDEKIMBO KIMOLO
2> AL-AMIN CHANDE
3> MWAMOYO HAMZA
4> GRACE SEBO MGAZA
5> HARUN ULOTU
F> ADDRESS:
THE MIRAGE HALL
1401 UNIVERSITY BLVD,
HYATTSVILLE, MD 20783
ZINGATIA HILI NI MUHIMU
UHALALI WA UPIGAJI/KUPIGA KURA TAREHE APRIL/15/2012 SAA 2:00PM (NANE MCHANA)
Watanzania wote ambao ni wakazi wa DMV (DC, VA, MD) wana haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa uongozi wa Jumuiya leo Jumapili Aprili 15 saa nane mchana. Ili kuthibitisha uhalali wako tafadhali uje na Uthibitisho wenye picha na Viambatanisho ambao utaonyesha kuwa ni mkazi wa DMV. Hili ni muhimu sana kukuwezesha kupiga kura yako. Tafadhalini sana tuzingatieni taratibu ili tuweze kufanikisha zoezi hili la kufufua Jumuiya yetu.
Asanteni sana
Givens Kasyanju
Mwenyekiti.
No comments:
Post a Comment