Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akisoma hotuba kwa niaba ya Mshauri Mwandamizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya KImbari nchini Rwanda, ambapo amehimiza nchi washiriki kuwa na imani na mahakama ya ICTR.
Picha Juu na chini ni Wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakisikiliza Lecture ya Profesa Chris Peter Maina wakati wa mjadala wawazi wa kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Mwaka 1994.
Balozi Mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Sano Lambert akitoa neno la shukrani na pia kuasa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutetea amani na maendeleo kwa faida ya vizazi vijavyo na maendeleo ya ukanda wa Maziwa makuu kwa ujumla.
Profesa Chris Peter Maina wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akielezea na kufafanua umuhimu wa Mahakama, akitolea mfano ya ICTR kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kijamii katika kuhakikisha haki inatendeka, haswa katika matukio kama ya uhalifu wa kivita.
Wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
Katibu Daraja la Kwanza wa Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania Bw. Ernest Bugingo akisisitiza jambo na kuwataka wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujifunza zaidi na kusoma makala za mauaji ya Kimbari kupitia mtandao.
Picha Juu na chini ni Wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
Na.Mwandishi wetu.
Wananchi wa Rwanda na Afrika Mashariki kwa Ujumla wametakiwa kulinda na kudumisha amani katika eneo la maziwa makuu kwa kuwa hiyo ndio misingi ya umoja na maendeleo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Msemaji na Mshauri Mwandamizi wa Kisheria wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda Bw. Roland Amoussouga, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vizo, amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda inasikitika na inatoa pole kwa wale walioathiririwa na vita vilivyotokea mwaka 1994na kuwa iko pamoja nao.
Aidha amesema tunapaswa kuweka kumbukumbu ya waliopoteza maisha na walionusurika , ambao kwa sasa wameathirika kimwili na kiakili.
Katika kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania.
Habari na picha kwa hisani ya MO Blog
No comments:
Post a Comment