Waandishi WetuMAASKOFU nchini wameonya kuenea kwa siasa za chuki na ufisadi wakisema ni mambo yanayoweza kulipeleka taifa kubaya.Aidha, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), imetaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ibadilishiwe majukumu na kushughulikia wizi wa mali za umma badala ya rushwa.
Kwa nyakati tofauti katika Ibada ya Pasaka jana, viongozi wa Kikristo walitumia madhabahu kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuunda Tume ya Kuratibu Maoni ya Mabadiliko ya Katiba.
Siasa za chuki
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa alisema wanasiasa wengi wanaeneza siasa za chuki hali inayolifanya taifa kuwa katika hali mbaya.
“Tumefikia mahali tunadhani hatuwezi kufanya siasa bila ugomvi wala kukashifiana, tulidhani wengine ni nafuu lakini sasa ni wote wanajiingiza kwenye siasa za ugomvi. Tumeona kwenye uchaguzi, hili linasikitisha kama taifa tumefika pabaya,” alisema Dk Malasusa.
Alisema kufufuka kwa Yesu Kristo kusaidie kurudisha uadilifu, uaminifu kwa viongozi na watendaji wa Serikali kwa sababu hayo yanawezekana.
“Haitoshi kuzungumzia miaka 2000 ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo bila kuzungumzia mabadiliko ya tabia kwa ajili kuhimiza uadilifu na uaminifu,” alisema Dk Malasusa.
Katibu Mkuu wa CCT Mchungaji, Dk Leonard Mtaita amependekeza Takukuru ibadilishwe kuwa taasisi ya kushughulikia wizi wa mali za umma ambao ni mkubwa, kuliko tatizo la rushwa nchini.
Alisema baadhi ya viongozi wasio waaminifu wameingia mikataba mibovu ambayo inawaletea wananchi maisha magumu. Aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kutoa maoni juu ya Katiba ya nchi katika Tume ilioundwa na Rais ili kurekebisha udhaifu.
Adhabu ya kifo
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa alisema sheria inayoruhusu adhabu ya kifo inakwenda kinyume na imani za Kikristo.
Alisema sheria za nchi zinasema anayemuua mwenzake kwa kukusudia adhabu yake ni kifo.
“Adhabu hii ni kielelezo cha binadamu kulipiza kisasi, Wakristo ichukieni adhabu ili hatimaye iweze kufanyiwa marekebisho,” alisema Nzigirwa.
Alilaani kitendo kinachofanywa na baadhi ya wanawake cha kutoa mimba na kuua viumbe ambao hawawezi kujitetea.
Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphone Mkude amewataka wazazi kulea familia zao katika maadili mema ili waje kuwa wazalendo wa nchi hii. Alisema baadhi ya viongozi wabovu waliopo hivi sasa ni matokeo ya malezi mabaya waliyolelewa na wazazi wao.
Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka Wakristo kuishi maisha yenye waledi yanayompendeza Mwenyezi Mungu.
Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya mkesha wa Sikuku ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam juzi, Kardinali Pengo alisema hakuna haja ya kuishi maisha ambayo yanamchukiza mwenzako.
Pengo alisema ni vyema kila mmoja akapenda kuishi maisha ambayo yatamfurahisha kila mmoja na siyo kuishi maisha ambayo yatamkwaza mwingine.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya, Evaristo Chengula amewataka viongozi na watoa huduma katika ofisi mbalimbali na jamii kwa ujumla, kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao kwa kuzingatia haki na usawa ili kuepusha vitendo vya ukiukwaji wa haki ikiwamo rushwa.
Askofu Chengula alitoa kauli hiyo wakati akiongoza Misa Takatifu ya pasaka iliyofanyika jana katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima, lililopo Mwanjelwa.
Tume ya Katiba
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Richard Kamenya amempongeza Rais Kikwete kwa kuunda Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza katika Ibada ya Misa ya mkesha wa Pasaka, Mchungaji Kamenya alisema safari ya Watanzania kuelekea kupata Katiba Mpya ni sawa na safari ya Waisrael ya kwenda Kanani ambako walikutana na majaribu mengi ambayo yalihitaji imani na uvumilivu ili kuyashinda.
Kwa upande wake, Kasisi wa Kanisa Anglikana la Mtakatifu John, Jackson Muya amewataka Wakristo kuiombea Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania iliyoteuliwa na Rais Kikwete ili iweze kutenda kazi yake kwa uadilifu, ikiwa ni hatua ya kwanza muhimu katika mchakato wa kuiwezesha nchi kupata Katiba Mpya ifikapo mwaka 2014.
Huko Zanzibar, Padri Stanley Lichinga wa Kanisa Kuu la Anglikana, Mkunazini amewataka Wakrito nchini kutunza utulivu na uelewano uliopo.
Akitoa ujumbe katika mahubiri yake, Padri Lichinga alisema amani, utulivu, umoja na umezungumzwa sana katika vitabu vitakatibu na kutakiwa wakristo wote kufuata nyayo za bwana Yesu ambaye alikubali kujitolea kwa ajili ya wakristo wote ulimwenguni na kwa kuwasamehe dhambi zao.
Padri Lichinga alisema ni vizuri wakati Wakristo wakasherehekea siku hiyo ya Pasaka wakazingatia maneno yalioandikwa katika Biblia na kutayafakari kwa kutafuta na kuachana na vitendo vyote viovu ambavyo vinakwenda kinyume na mafundisho.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Morogoro, Godfrey Sehaba amewataka Watanzania kuacha kutaka utajiri wa haraka kwa kutumia waganga wa kienyeji na badala yake, wajishughulishe na ujasiriamali.
“Waganga wa kienyeji wamekuwa wakidanganya watu kuwa watapata utajiri kupitia viungo vya binadamu, huwezi kupata utajiri kamwe kupitia miujiza ni lazima kujishughulisha ndipo utatajirika,’’ alisema.
Askofu Godfrey Mhogolo wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Dodoma amewataka wanasiasa kuacha kutukana na badala yake waeleze sera za vyama vyao.

Alisema wananchi wana hamu ya kusikia sera za vyama hivyo namna zitakavyowakomboa badala ya kusikia matusi kila siku… “Wananchi wamechoshwa na misamiati ya matusi kwenye majukwaa, waelezeni sera zenu.”
Mwananchi
No comments:
Post a Comment