Na Mwandshi Wetu
MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika
mei 4 katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam akizungumza
na waandishi wa habari Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Ngumi Rajabu
Mhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki
michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.Aliwataja
baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Class
atakaezichapa na Idi
Mnyeke, Amiri Macho atazidunda na West Scorpion,Charo Issa na Hamis
Nassoro,Athumani Sadara na Abuu Mtambwe, Hassan Mijugu ataoneshana
kazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal Ignus.
Pamoja na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti tofauti
vijana wengi
wamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau wa
mchezo wa masumbwi
kufanikisha mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kinyogoli Fondition kwa
ajili ya kuwapanga
katika viwango mbalimbali vya ubora wa wachezaji,
Alitaja baadhi ya maitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezaji
wakati wakiwa
ulingoni,zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa mbalimbali
yatakayotumika kwa
ajili ya kuwapatia mabondia huduma ya kwanza alisema Super D.
Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidi mashindano hayo kwa namna moja au
nyingine anaweza
kuwasiliana
na kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 au
unaweza fika katika klabu
ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza kuwasiliana
na kocha Super D
0713/0787-406938 au unaweza fika Klabu ya Ashanti Iliyopo Ilala Soko
la Mitumba kwa mawasiliano zaidi
No comments:
Post a Comment