Mpenzi msomaji wangu, juzi nilikuwa nazungumza na rafiki yangu kuhusiana na maisha yake ya ndoa. Nimejifunza mengi kupitia kwake lakini kubwa ambalo nimeona ni vyema ‘nikashea’ na nyie kupitia safu hii ni hili la wanandoa kuridhishana katika tendo la ndoa.
Hakuna asiyefahamu umuhimu wa mke na mume kukutana faragha na kupeana ‘mambo’ kwa raha zao. Kila mmoja anapenda hivyo na kama atatokea anayelichukia tendo hilo, huyo atakuwa punguani. Tukumbuke tu kwamba mapenzi ni nguzo madhubuti ya kuifanya ndoa idumu.
Hata hivyo, katika maisha ya sasa kuna mambo yanajitokeza na kusababisha baadhi ya wanandoa kushindwa ‘kupafomu’ inavyotakiwa wawapo faragha na wapenzi wao. Wakati nazungumza na rafiki yangu huyo aliniambia kuwa, miongoni mwa mambo yanayomkosesha amani katika maisha yake ya ndoa ni mkewe kuhisi ana mwanamke mwingine nje.
“Eti ananiambia siku hizi ‘dozi’ ninayompatia ni tofauti na ilivyokuwa zamani. Ananiambia nina kimada anayenizuzua. Anashindwa kujua kuwa hiyo imetokana na kazi ninayoifanya.
“Hebu fikiria unafanya kazi hadi muda wa ziada na kurudi nyumbani ukiwa umechoka kupita maelezo, unadhani unaweza kumridhisha mkeo inavyotakiwa? Hiyo ni changamoto inayonikabili kwa sasa,” anasema rafiki yangu huyo.
Maelezo ya rafiki yangu huyu ni kilio cha wanaume wengi hasa wanaofanya kazi ngumu na zile zinazotumia akili nyingi. Kiukweli kama nilivyosema, hakuna asiyependa kufanya tendo hilo na kumridhisha mke wake lakini zinapokuwepo sababu za msingi za kushindwa kufanya hivyo, iwe rahisi kwa mwingine kuelewa.
Nasema hivyo kwa kuwa, udhaifu kidogo katika tendo la ndoa haiwezi kuwa sababu ya kuwakosesha amani kiasi cha mmoja kufikiria kumuacha mwenzake. Ikiwa mwenza wako hakupi kama ilivyokuwa huko nyuma, ni suala la kukaa na kuangalia chanzo ni nini?
Si bure, ni lazima kutakuwa na sababu za msingi. Itakuwa ni tatizo kubwa kama utachukulia kwamba chanzo cha yote hayo ni mtu wako kuwa na kiburudisho kingine.
Yawezekana ikawa hivyo kweli lakini usiwe na jibu hilo bila kumchunguza vizuri na kubaini ukweli. Nasema hivyo kwa kuwa, unaweza kufikiria hivyo kumbe sababu ni maradhi, umri kwenda au kusumbuliwa na msongo wa mawazo.
Kumbuka mapenzi siyo chakula na mapenzi si kitu cha kufanya kwa kukomoana. Tatizo la baadhi ya wanawake wanataka wanapokutana na waume zao wapewe ‘mambo’ mpaka waseme wametosheka. Jamani, kila siku siyo Ijumaa! Kuna siku mwili na akili vinakataa kabisa, tukubaliane na hali hiyo!
Kingine ninachotaka kukizungumza leo ni kwamba, maisha ya sasa yana changamoto nyingi. Uchu wa kuwa na mafanikio kwa kila mtu umesababisha wengi kutotilia maanani sana mambo ya mapenzi.
Ndiyo maana unaweza kukuta mwanaume anatafuta maisha mazuri kwa kutumia muda wake mwingi kutafuta fedha kuliko kuwa faragha na mke wake. Hilo lisiwe tatizo la kuweza kuwaachanisha.
Kikubwa ni kupeana furaha kwa kiasi kinachowezekana na kujadiliana pale ambapo unahisi kuna upungufu. Mpenzi wako akishindwa kukutana na wewe kwa madai kuwa siku hiyo kachoka kutokana na kazi nyingi alizofanya, muelewe na wala usiwe mkali.
Siku nyingine akikupa mapenzi pungufu tofauti na alivyokuzoesha, wala usiwe na majibu yako kichwani kwamba eti anakusaliti. Kwa kufikiria hivyo utakuwa unatengeneza bomu ambalo mwisho wake hauwezi kuwa mzuri.
www.globalpublishers.info.
No comments:
Post a Comment