ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 6, 2012

NAJITOA KUGOMBEA URAIS DMV NA MU-ENDORSE LOVENESS FOR PRESIDENT


Loveness Mamuya
Ningependa kuwatangazia Watanzania wenzagu kupitia kwenu kuwa, Najitoa katika kugombea Urais/Uongozi wa Jumuiya yetu ya Watanzania.
Na nawatakia kila la heri wote wanaogombea Uongozi wa Jumuiya yetu, na natumaini tutapata Uongozi bora na wenye mwelekeo wa mbeleni
katika mafanikio makubwa ya Jamii ya Watanzania "Wanajumuiya" , Nchi yetu tukufu na wananchi wake.
Na napenda kuwashukuru wote walio jitolea na walio kuwa tayari kujitolea katika kushiriki nami katika Ugombeaji katika Jumuiya.

  Hivyo basi, kama Mwanajumuyia na kama Wanajumuiya wengine napenda kumuunga Mkono Dada yetu mpendwaLOVENESS.
Nanatumaini wanajumuiya wengi watashirikiana nami katika kumuunga mkono dada yetu, mwanaetu LOVENESS.
Kwa kipindi kilefu, LOVENESS amaweza kufanya vitu vingi katika Jumuia yetu, kushirikiana na Watanzania wenzetu katika shughuli mbalimbali
za raha, shida. Mfano, kwenye misiba, Loveness amekuwa mstari wa mbele, Kusaidia nyumbani Tanzania - Watoto yatima na kweyeshughuli
za sherehe mbalimbali. Na mengine mengi ambayo ameweza kuyafanya, Na natumaini kabisa kama akipewa Uongozi wa Jumuiya yetu
atafanya makubwa zaidi na kuendeleza aliyo kuwa ameisha yaanza.

Napenda kuwashukuruni nyote kwayote.

Aksanteni

Givens Kasyanju

17 comments:

Anonymous said...

WOOOOOOOOOOOOW!! SASA MMENENA NI VIZURI MMETUPA MWANAMKE KWA SASA TUNAHITAJI MABADILIKO DADA LOVENESS NAKUOMBA FUNGA MKANDA WEKA PAMBA MASIKIONI NAJUWA UNAWEZA KAZI NI NGUMU LAKINI NAKUAMINIA KURA YANGU NA WATOTO ZANGU UNAYO KILA LA KHERI DADA

Anonymous said...

Dada hua unajitahidi sana kwa shughuli,mbalimbali za jamii,kwa hilo hakuna ubishi,unashirikiana na watu wote bega kwa bega bila wasiwasi,kura yangu umepata.

Anonymous said...

Dada Loveness kura yangu na familia yangu yote kwako. Wanawake tukiwezeshwa tunaweza.

Anonymous said...

Loveness kusema kweli anatufaa sana. Hana moyo wa hiana na anasaidia sana watu wakati wa matatizo. Kura yangu mimi na familia yangu umepata.Pia hatjawahi kuwa na president wa kike.Dada tunakushukuru kwa kugombea. Mungu akubariki.

Anonymous said...

HONGERA SANA DADA. HAKIKA WEWE NI MFANO WA KUIGWA NA UNATUFAA SANA.

Anonymous said...

Loveness wishing you all the best our dear. We are 100% sure that you will lead our community well. God Bless you

Anonymous said...

swali la kizushi tuu wale hetars wa dmv mtaenda kupiga kura au ngoja tuone ??maana kwatu wa dmv mnatia aibu ushirikiano zero mabishoo wengi wasio na ushirikiano

Anonymous said...

Chamecha mae. Ninakutakia mafanikio mema siku ya uchaguzi, Marangu na Dodoma hawatalala hiyo siku ndao mono wa Mamuya

Anonymous said...

Hapo umeongea ndugu, wengi wetu hapa tumezidi ubishoo wa kwenda kwenye starehe tu ila vitu muhimu kama hivi hatuna muda navyo. Kukitokea misiba, wagonjwa na matatizo mahudhurio hafifu lakini ikitokea sherehe kila mtu ata call off kazini ili aende. Inasikitisha sana jamani tushirikiane

Anonymous said...

kura yangu umepata dada. cha msingi nakuomba uwe daraja kwa gap lililopo la watanzania hapa DMV ,too much hating,maendeleo binafsi zero,maendeleo kama watanzania kwa ujumla zero,please tusaidie tuungane tuwe kitu kimoja , na tupendane!waafrika wenzet haoa USA wako fit sana uki compare na sisi !!

Anonymous said...

LUKE, TUNAOMBA PICHA ZA WAGOMBEA WOTE NA NAFASI WANAZOZIGOMBEA. ASANTE.

Anonymous said...

mimi mdau wa vijimambo na nakaa houston je naweza kupiga kura? Mpwa maana huyu sister ningependa sana ashinde dc mpo hapo mimi nashangaa sana mji mkubwa hamna jumuiya kumbe ?

Anonymous said...

100%Unafaa kabisa na kuja kupiga kura
100% kazi utaiweza
50% watanzania kufanyakazi nao ni shada sana
70%watu wanaweza kujitokeza sema
ushauri dada loveness je watanzania tunashukrani?? hapo utatata je utavumilia
kero zao?mmmh goodluck mimi nitawahi sana hiyo siku

Anonymous said...

Tunaomba kuwajua wagombea wengine na nafasi zao

Anonymous said...

Unaona wachagga wameanza atakuwa rais wa wachagga au wa watanzania wote? anaonekana kwenye sherehe zaidi vifo na matatizo mengine kama sio mchagga haonekani. Alikuwa mstari wa mbele kwenye msiba wa wachagga na wapare. Sisi wa kusini hatutambui.

Anonymous said...

Kura zinapigwa Lini na wapi?

Anonymous said...

hIVI MNA HABARI HII KAZI NI YA KUJITOLEA?MUDA ,AKILI NA MENGINEYO?HAWALIPWI HAWA TUWAUNGE KONO.