Baadhi ya watoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine , aliyekuwa Waziri Mkuu,ambaye alifariki dunia Aprili 12, mwaka 1984 eneo la Wami Ruhindo, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, miongoni mwa watoto hao ( wakwanza kulia ) ni Mbunge wa Viti Maaalumu, Namelok Sokoine.
Waziri Mkuu wa zamani aliyejihudhuru Edward Lowassa ( kulia) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe , baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kanisa la Kigango cha Wami Sokoine , kuhudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 28 ya Kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine , kilichotokea Aprili 12, 1984 eneo la Wami Ruhindo, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
Mbunge Amos Makalla ( kushoto) akisalimiana na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa katoliki Jimbo la Morogoro , baada ya kumalizika ibada ya misa ya kumwombea hayati Sokoine
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( kulia) akisalimiana na Askofu Telesphor Mkude , ( kushoto) baada ya kumaliza kusoma ibada ya misa ya kumkumbuka ya kumwombea Marehemu , Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine , aliyetimiza miaka 28 tangu kifo chake kilichotokea Aprili 12, 1984 eneo la Wami Ruhindo, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Pinda alikuwa ni mgeni rasmi katika tukio hilo.( Picha na John Nditi).
No comments:
Post a Comment