Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiahirisha Bunge hivi karibuni, Bunge hilo lilitawaliwa na hoja ya uwajibikaji ambapo wabunge walitaka Mawaziri waliofanya vibaya katika wizara zao wajiuzulu
SHINIKIZO la kutaka mawaziri wanane wajiuzulu limezidi kushika kasi baada ya Chadema kuitisha kikao cha Baraza Kuu kutaka baraka zake za kuitisha maandamano huku wanaharakati wakitoa taarifa wakiwataka viongozi hao waachie ngazi.
Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa kumekuwa na shinikizo la kutaka mawaziri wanane kujiuzulu baada ya wizara zao kutajwa kuhusika na ufisadi katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi (CAG), huku baadhi wakionekana kuwa na maslahi binafsi katika wizara zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wanaharakati wameitaka Serikali kuwawajibisha mara moja mawaziri, manaibu waziri na watendaji wakuu wa Serikali na mashirika ya umma ambao wametajwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma au kushindwa kusimamia rasilimali za nchi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Anna Kikwa ilisema ni muhimu Serikali iboreshe mifumo ya kusimamia rasilimali za nchi ili wananchi wote waweze kufaidi keki ya taifa.
“Ili kuboresha dhana ya uwajibikaji na utawala bora unaozingatia misingi ya haki za binadamu, ni muhimu Serikali ikafanya hayo," alisema Kikwa.
Alisema mara kadhaa, wabunge wamekuwa wakiweka kando itikadi zao za kisiasa na kusimamia kwa dhati dhana ya uwajibikaji katika vyombo vya Serikali.
“TGNP kwa muda mrefu wamekuwa wakipinga ubadhirifu wa fedha za umma na kudai haki ili kutokomeza ufisadi uliokithiri, lakini bado ufisadi umezidi kushamiri hasa katika wizara na taasisi za umma,” alisema na kuongeza:
“Kuendelea kwa ufisadi ni aibu kwa Serikali iliyoko madarakani, TGNP tuko mstari wa mbele kushinikiza rasilimali za taifa ziwanufaishe wananchi wote, hasa walioko pembezoni. Kamwe hatutanyamazia aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya wananchi zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.”
Baraza Kuu Chadema
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema jana kwamba kikao cha Baraza Kuu kitafanyika Jumamosi ijayo kupokea na kujadili ajenda ya hali ya siasa nchini na kuamua hatua za kuchukua ikiwemo maandamano.
Mnyika alisema tayari chama chake kimeanza maandalizi ya kuunganisha nguvu ya umma kushinikiza mawaziri wanaotuhumiwa wajiuzulu baada ya Serikali kushindwa kufanyia kazi hoja iliyoibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
“Chadema inaongozwa kwa fikra za falsafa ya nguvu ya umma na inaamini kwenye itikadi za siasa zilizo juu ya vyama zenye kusimamia maslahi ya taifa,” alisema Mnyika na kusisitiza kuwa Serikali inaposhindwa kulinda ufisadi, umma unapaswa kuungana katika kuiwajibisha.
“Tulifanya hivyo Septemba 15, 2007, tulipotoa orodha ya mafisadi na tuko tayari kufanya hivyo sasa. Tayari mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe alishatangaza bungeni wiki iliyopita kuwa tunarudi kwa wananchi kutaka uwajibikaji wa Serikali,” alisema Mnyika na kuongeza:
“Pia Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa katika mikutano yake ya hadhara aliyofanya Mwanza, amerudia kutoa kauli juu ya suala hilo akikumbushia wito aliotoa mwaka 2011 wa kumtaka Rais Kikwete kulivunja Baraza la Mawaziri.”
Mnyika alisema tayari chama hicho kimeshaanza maandalizi kutaka hatua za uwajibikaji, baada ya kuona Rais hakuzingatia ushauri uliotolewa na wabunge ambao alisema ni muhimu kwa maslahi ya taifa.
Mukama
Katibu Mkuu CCM, Wilson Mukama amekanusha madai yaliyotolewa na Mbunge wa Mwibara kwa tiketi ya chama hicho, Alphaxard Lugola ambaye alidai kwamba kiongozi huyo alimtishia siku moja baada ya kusaini karatasi ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mukama alisema jana kwamba amesikitishwa na taarifa huku akisisitiza kuwa wabunge wote wa chama tawala, wana haki na uhuru wa kutoa maoni yao kwa kuwa wametumwa kuwawakilisha wananchi.
Mukama alisema hawezi kumtisha mbunge yoyote kwa kuwa wabunge wa chama chake wanatimiza wajibu wao kama wanavyostahili hivyo, hawezi kuwatolea vitisho.
Awali, Lugola alikaririwa na gazeti hili akisema usiku wa kuamkia Jumapili, siku moja baada ya kusaini karatasi ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu alipokea simu kutoka kwa Mukama huku akimtolea maneno makali kutokana na hatua yake hiyo.

Mwananchi
No comments:
Post a Comment