ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 26, 2012

Tovuti ya Sekreterieti ya Ajira yazinduliwa


Waziri wa Nchi,
 Ofisi ya Rais (Menejimenti
 ya Utumishi wa Umma),
Hawa Ghasia
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, imeitaka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kutoa ajira bila upendeleo wakati idara mbalimbali za serikali zinapotangaza nafasi za kazi ili kupata watumishi wenye sifa serikalini.
Waziri Ghasia aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Tovuti ya Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma inayojulikana kwa www.ajira go.tz
Alisema Sekretarieti hiyo sasa inatakiwa kuachana na mazoea ya kutoa ajira kwa kuendekeza ukabila na matokeo yake wanajikuta wanatoa ajira kwa watumishi wasiokuwa na sifa na kushindwa kukidhi malengo ya serikali.
Aidha, alitaka Sekretarieti hiyo kutumia tovuti hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali zinazohusiana na mchakato wa kutangaza nafasi za kazi, kusaili waombaji wenye sifa na kuwapangia vituo vya kazi kwa watakaokuwa wamefaulu.

Mwenyekiti wa Sekretarieti hiyo, Bakari Mahiza, alisema suala la kuwa na watumishi wenye sifa na ujuzi wa kutosha katika utumishi wa umma ni muhimu katika dunia ya leo ambapo kuna ushindani mkubwa wa kimaendeleo na kiteknolojia.
Mwisho.
Vifo vya malaria vyapungua
Na Ninaeli Masaki
MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, amesema Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kutokana na matumizi vyandarua vyenye dawa.
Dk. Bilal aliyasema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya malaria duniani yaliyofanyika jijini, ambapo katika sherehe hizo pia alizindua ripoti ya utekelezaji wa mikakati ya malaria Tanzania Bara.
Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Hadji Mponda, alisema, matumizi ya vyandarua sahihi vyenye dawa pamoja na dawa sahihi ya mseto kwasasa yameongezeka kwa kiasi kikubwa.
Mponda aliongeza kuwa vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kutokana na matumizi ya vyandarua pamoja na dawa halisi za mseto.
CHANZO: NIPASHE

No comments: