Ndugu Wanajumuiya,
Kama tulivyowafahamisha hapo awali kuwa kazi mliyotutuma imekamilishwa. Tuna washukuruni wote mlioleta na kutuma mapendekezo yenu kutokea mwanzo mpaka mwisho wa ukamilishaji wa Katiba mpya. Maoni yenu yote yalipokelewa na kufanyiwa kazi ndani ya Katiba, tunashukuru sana kwa mchango na muda wenu mliojitolea kwa nia ya kujenga Jumuiya yetu ya Watanzania DMV.
Hivyo basi, imetufikisha katika hatua kubwa naya mwisho ya kuindeleza mbele Jumuiya yetu. Na kama tunavyojua kuwa kwa sasa hivi hatuna Jumuiya na kamati iliyofanyia marekebisho katiba haina Fedha, Kutokana na hali hiyo, Wanakamati tumependekeza kama ifuatavyo
- Tutakuwa na Mkutano mkuu mmoja ambao utashughulikia maswala makuu mawili:
1. Shughuli ya kwanza itakuwa ya kupitia na kupitisha Katiba.
2. Shughuli ya pili itakuwa ya uchaguzi mkuu, tutachagua viongozi wa Jumuiya.
Mkutano Mkuu utafanyika tarehe 04/15/2012 saa 8 mchana ( 2:00pm). Katika
Ukumbi wa
MIRAGE HALL
1401 UNIVERSITY BLVD
HYATTSVILLE, MD 20783
1 comment:
DJ...siku hiyo tutahitaji kuchagua kamati ya uchaguzi...kamati iliyopo sasa ilipewa jukumu la kusimamia katiba na sio uchaguzi. Hatuna imani nayo kwani kiongozi wake tayari amemuindozi mmoja wa wagombea. Ongeza hili kama moja ya ajenda ya jumapili.
Mdau DMV
Post a Comment