ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 27, 2012


UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 WASHINGTON D.C.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar atafanya mkutano na Watanzania tarehe 11 Mei 2012 mjini Houston, Texas. Watanzania waishio maeneo ya karibu kwenye miji ya Houston, Dallas, Oklahoma, Kensas, Lousiana, New Mexico na kwingineko, wanaombwa kufika kwa wingi siku hiyo.

Aidha, Mhe. Balozi ataambatana na Afisa wa Uhamiaji kutoka ubalozini Washington DC ili kutoa huduma za kikonseli ikiwemo ile ya kupokea maombi ya kubadili pasi za zamani za kusafiria ili kupata mpya (New generated Machine Readable) wakati wa ziara hiyo.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia tarehe 11–13 Mei, 2012. Anuani ya mahali ambapo mkutano na zoezi la pasi litafanyika, itatangazwa na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Mjini Houston, Texas.


KARIBUNI WOTE

Imetolewa na:

Ubalozi wa Tanzania, Washington D.C,
1232 22nd St. NW, Washington D.C 20037
Telephone: (202)884-1080, (202)939-6125/7
Fax: (202)797-7408
Tarehe: 27.03.2012

No comments: