ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 27, 2012

Walimu wajisaidia nyumba za jirani-Habari Leo

BAADHI ya shule za msingi wilayani Lindi hazina vyoo na kusababisha wanafunzi na walimu kujisaidia katika nyumba ambazo zipo karibu na shule hizo na kwenye mito. 

Hayo yalielezwa jana kwenye mkutano wadau wa elimu ulioitishwa na Shirika la Vyama vya Hiari na Maendeleo ya Jamii (TACOSODE) na Policy Forum uliowashirikisha wananchi na viongozi wa halmashauri, wakiwamo madiwani, wakuu wa Idara katika Kata ya Mtama. 

Wakichangia juu ya maendeleo ya elimu hususani katika shule za msingi, baadhi ya wananchi walizungumzia ukosefu wa vyoo, uhaba wa nyumba za walimu, madawati na madarasa. 

Mkazi wa Kijiji cha Mtama, Hamisi Saidi (Kitangali) alisema Shule ya Msingi ya Mihogoni wanafunzi wake wanakwenda kujisaidia kwenye Mto wa Lukuledi ambao wananchi huutumia kwa kwa ajili ya maji ya kupikia, kuoshea vyombo, kufulia na kuoga na hata kunywa. 

Alishauri kutokana na Shule hiyo ya Msingi Mihogoni kutokuwa na vyoo viongozi wa Serikali ya Kijiji, Kata kuweka utaratibu wa kusimamia fursa zilizopo mojawapo michango kwa wazazi wanayoitoa Sh 1,000 kwa ajili ya kujenga vyoo itumike ipasavyo tofauti na sasa zinatolewa fedha hizo, lakini hakuna choo.

No comments: