Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar
Balozi wa Tanzania Marekani, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar atafanya mkutano na Watanzania mjini Houston, Texas. Watanzania waishio maeneo ya karibu kwenye miji ya Houston, Dallas, Oklahoma, Kensas, Lousiana, New Mexico na kwingineko tarehe 11 mei 2012, kuanzia saa kumi na mbili jioni kwa saa za Texas. Tunaombwa kufika kwa wingi siku hii katika anuani ifuatayo:
9301 W. Bellfort Ave. Turquoise Center, Houston, Texas, 77031
Mhe. Balozi ataambatana na Afisa wa uhamiaji kutoka ubalozini Washington DC ili kutoa huduma ya kubadilisha pasi za kusafiria. Huduma hii itatolewa kuanzia tarehe 11-13 mei 2012 katika anuani hiyo hiyo hapo juu.Jiorodheshe kwa kutuma email yenye kichwa cha habari PASS na ambatanisho la JINA KAMILI katika email, tzhoustoncomm@gmail.com. Huduma itatolewa kwa kufuata/kuita majina ya waliojiorodhesha kwanza. Kwa gharama/nyaraka hitajika katika zoezi la pasi Bofya hapo chini:
'Mawasiliano kati ya Viongozi na Wananchi ni Nguzo Muhimu ya kuleta Maendeleo katika Nchi.'
Watanzania wote karibuni!
Novastus Simba, Mwenyekiti
Jumuia ya Watanzania Houston
cell: 832-208-8344
No comments:
Post a Comment