Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar amezindua rasmi programu ya kiswahili inayofundishwa na Chuo Kikuu cha Indiana.
Porgramu hii (ya kufundisha Kiswahili) ni ya kwanza nchini Marekani ambapo wanafunzi wanaosoma Kiswahili wanapata ufadhili kutoka Serikali Kuu ya Marekani. Wanafunzi hao pia watapata fursa ya kusoma Chuo Kikuu cha Zanzibar kwa mwaka mmoja kama sehemu ya programu hiyo.
Kwa picha zaidi Bofya Read More
Picha kwa hisani ya Mindi Kasiga
1 comment:
Tunampongeza balozi Mwanaidi na serikali ya Tanzania kwa jitihada wanazozifanya za kufanya lugha ya kiswahili kutambulika kimataifa
Natoa pongezi hizo kwasababu mabara mengine yanajivunia lugha zao kwa maana hiyo natoa mwito kwa viongozi wote wa Afrika kuhamasiha lugha hii ifundishwe katika vyuo vikuu barani Afrika na ikiwezekana ije kuwa lugha ya kuwaunganisha Waafrika
Hii itamuenzi marehemu Julius Kambarage alipokutana na viongozi wa Afrika hususani Raisi wa Ghana Kwame Nkuruma kuhusu kuinganisha Afrika.
Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania
Post a Comment