Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mji mdogo wa Ruaha, wilayani Kilosa mkoani Morogoro walifanya vurugu zilizosababisha kufungwa kwa barabara kwa saa tano.
Inadaiwa kuwa wafuasi wa Chadema walikwua wakishinikiza mgombea wao wa uenyekiti wa mji huo kutangazwa kuwa mshindi, baada ya kuharishwa kwa uchaguzi wake.
Habari zinasema kuwa katika vurugu hizo wafuasi hao walichoma moto matairi ya magari barabara, kupasua vioo vya magari na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospitalini ya Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.
Vurugu hizo zilianza saa tano asubuhi wakati wafuasi wa Chadema walipokusanyika katika ofisi za mji huo mdogo kutaka maelezo ya kwanini uchaguzi uliopangwa kufanyika juzi wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Tito Haule wa CCM kufukuzwa mwaka jana kwa madai ya ubadhilifu wa fedha za umma.
Fujo hizo zilianza juzi baada ya kushindwa kufanyika kwa uchaguzi huo pasipo kuwepo kwa taarifa zozote hali ambayo ilizua hasira kwa wananchi waliokuwa wamejitokeza kwa ajili ya kupiga kura.
Kutokana na hali hiyo, wafuasi wa Chadema jana walimua kukusanyika katika ofisi za mji huo mdogo kutaka maelezo kwanini uchaguzi huo umeshindwa kufanyika na kuelezwa kuwa Mkurugenzi ameahirisha baada ya mgombea wa Chadema kuwekewa pingamizi na mgombea wa CCM.
Majibu hayo yalisababisha wafuasi hao kuanza kufanya vurugu huku walimtuhumu Diwani wa Kata ya Ruaha (CCM), Rachel Nyangasi, kuwa ndiye aliyekwamisha kutokufanyika uchaguzi huo.
Diwani huyo alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kutuhumiwa kukwamisha uchaguzi huo. Mmoja wa wananchi alijitambulisha kwa jina Ally Athumani, alisema vurugu hizo zilikuwa zikifanywa na wafuasi wa vyama vya CCM na Chadema kuhusiana na uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Amer Mbarak, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kueleza kuwa zilisababishwa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kusitisha uchaguzi huo bila taarifa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment