Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Jordan Rugimbama |
Rugimbana aliamua kuitisha mkutano na wanamgambo hao ambapo aliwapa ruhusa ya kueleza matatizo yao ili ayasikilize na kuyafanyia kazi.
Mgambo mmoja aliyejulikana kwa jina la Barnabas Ntumbuka alisema chanzo cha mgogoro huo ni tangazo la mkurugenzi huyo ambalo alilitoa Aprili 30, mwaka huu ambalo iliwataka askari hao wenye mkataba wa miezi mitatu kuwa mkataba wao umemalizika rasmi tarehe hiyo hivyo warejeshe vifaa.
“Kufuatia tangazo hilo, tuliona kuwa hatukutendewa haki kwani haukuwa utaratibu kuweka tangazo ila walitakiwa watuandikie barua hivyo kwa kuwa sisi hatukuandikiwa barua tunaona kuwa sisi ni wafanyakazi halali wa manispaa hiyo,” alisema Ntumbuka.
Aidha, alisema kuwa walitegemea kusimamishwa kwao kungeendana na stahiki zao ambazo ni malipo ya ziada, malipo ya NSSF, malipo ya likizo pamoja na mapunjo ya mshahara.
Magnius Lupindo, alilalamikia utaratibu unaotumika katika kutoa ajira ambapo alidai utaratibu uliopo sasa ni wa upendeleo kwani wapo mgambo ambao wana miaka 15 sasa hawajapata ajira za kudumu.
Rugimbana baada ya kuwasikiliza, alimtaka mwanasheria na Mkurugenzi Fuime kuongoza kwa kufuata sheria na taratibu, na kuitisha mkutano mara moja ili kujadili matatizo mbalimbali yaliyojitokeza, baada ya kubaini kuwa hakuna mkutano wowote uliowahi kufanyika kati yao.
“Naomba kesho (leo) mwanasheria ukutane na wanamgambo hawa ili kuweza kuwatatulia matatizo yao kwani chanzo cha mgogoro huo kinatokana na pande hizi mbili kutokukutana kuzungumzia matatizo yaliyopo,” alisema Rugimbana.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment