Kikosi cha Chelsea kilichoanza
Mchezaji Philipp Lahm wa FC Bayern Muenchen akijaribu kuchanja mbuga huku wachezaji wa Chelsea Ashley Cole (shoto) na Juan Mata wakijaribu kumpunguza kasi katika mechi ya fainali ya Club bingwa ya UEFA ilyochezwa Jumamosi May 19, 2012 kwenye uwanja wa Fussball Arena Mjni Munich Ujerumani.
Alikua atumwi mtoto dukani David Luiz wa Chelsea akimdhibiti Thomas Mueller wa FC Bayern Muenchen katika mpambano wa fainali wa Club Bingwa Ulaya uliochezwa Jumamosi May 19, 2012, Munich, Nchini Ujerumani.
Wanaume wanapopambana ziumiazo ni nyasi, Juan Mata Mchezaji wa Chelsea akiwa chini baada ya kukwatuliwa na Franck Rebery wa FC Bayern Muenchen (bukta # 7) huku Thomas Mueller (kulia) akiwa anaangalia kwenye mpambano wao wa fainali uliochezwa Jumamosi May 19, 2012 Mjini Munich, Nchini Ujerumani.
Kiungo wa Chelsea na Timu ya Taifa ya Uingereza, Frank Lampard akigombea mpira na Thomas Mueller wa FC Bayern Muenchen katika fainali ya Club bingwa Ulaya iliyochezwa Jumamosi May 19, 2012, Munich Nchini Ujerumani.
Wachezaji wa FC Bayern Muenchen wakimpongeza Thamas Mueller baada ya kuipataitia timu yake bao la kuongoza kunako dakika ya 83 ya mchezo.
Didier Drogba na wachezaji wenzake wa Chelsea wakishangilia bao la kusawazisha kunako dakika ya 88 ya mchezo, baada ya kuwa nyuma kwa bao 1 walilofungwa kunako dkk ya 83 ya mchezo.
Wanadarajani ngoma ilikua inaishia hapa lakini Petr Cech akapangua penati ya Arjen Robben wa FC Bayern Muenchen kunako dkk ya 90.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia Penati ya mwisho ya ushindi aliyofunga Didier Drogba katika mpambano wa fainali ya Club Bingwa Ulaya baada ya 120 kutopatikana mshindi ndipo zilipopigwa penati tano, tano na Chelsea kupata 4 - 3 dhidi ya FC Bayern Muenchen.
Mkula wa Darajani, Roman Abramovic (aliyenyanyua kombe) akiwa mwenye furaha baada ya Chelsea kuchukua ndoo ya Club Bingwa Ulaya anaepiga makofi kati tai ya bluu ni Chencellor Of The Exchequer, George Osborne.
Picha kwa hisani ya Mike Hewitt/Getty Images Europe
No comments:
Post a Comment