ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 3, 2012

Maiti 7 wa ajali ya NBS watambuliwa-Habari Leo

MAITI saba kati ya wanane wa ajali ya basi la NBS iliyotokea juzi wilayani Igunga mkoani Tabora, wametambulika wakati majeruhi wanne wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya. 

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Dk. Joseph Kisali alisema jana kwamba miili ya marehemu saba imetambuliwa na ndugu zao na jitihada za kuichukua zinaendelea. 

Dk. Kisali aliwataja marehemu kuwa ni Dickson Nassani, Zainabu Hamudu, Anna Kisima, Msemo Advocatus, Kalekwa Ramadhani ambaye alikuwa na mtoto wake wa kiume na aliyefariki dunia katika ajali hiyo aliyetambulika kwa jina mmoja la Saidi pamoja na mwingine pia aliyetajwa kwa jina la Msukuma wa Mwanza. 

Alisem,a majeruhi waliopata ruhusa kulingana na hali zao ni 32 huku wanne wakibaki hospitalini hapo kuendelea na matibabu. Alisema hali zao ni nzuri. 

Alisema, majeruhi wengine wanne wenye hali mbaya, wamepelekwa Bugando kwa matibabu zaidi kutokana na uhaba wa vifaa katika hospitali hiyo ya wilaya. 

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Iddi Hussein ambaye ni dereva wa basi hilo, Romana Rabia na Happy Saidi. 

Basi la NBS aina ya Scania lenye namba T978 ATM lililokuwa likitokea mkoani Tabora kwenda Arusha, lilipaya ajali juzi asubuhi eneo la Jineri wilayani Igunga na kusababisha vifo vya watu saba na kujeruhi 54. 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Antony Rutta, chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa matairi ya mbele na kwenda kuparamia mti.

No comments: