Washington DC
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewahimiza wadau afya na lishe kutoka
mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na taasisi za Kitanzania na
Serikali kwa ujumla ili kuinua afya ya mtoto na mama nchini Tanzania.
Aliyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa pamoja na NGO sita za
kimarekani zinazofanya kazi mbalimbali nchini Tanzania kwenye masuala ya
lishe na afya tarehe 18 Mei 2012. Taasisi zilizohudhuria mkutano huo ni
Malaria No More, Health Overseas Volunteers, Path International, Save the
Children, Global Health and Diplomacy na Africare International,
uliofanyika pembezoni na mikutano ya Rais Kikwete kuhusu masuala ya
usalama wa chakula na lishe duniani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewahimiza wadau afya na lishe kutoka
mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na taasisi za Kitanzania na
Serikali kwa ujumla ili kuinua afya ya mtoto na mama nchini Tanzania.
Aliyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa pamoja na NGO sita za
kimarekani zinazofanya kazi mbalimbali nchini Tanzania kwenye masuala ya
lishe na afya tarehe 18 Mei 2012. Taasisi zilizohudhuria mkutano huo ni
Malaria No More, Health Overseas Volunteers, Path International, Save the
Children, Global Health and Diplomacy na Africare International,
uliofanyika pembezoni na mikutano ya Rais Kikwete kuhusu masuala ya
usalama wa chakula na lishe duniani.
Katika hotuba yake na taasisi hizo, Mama Salma Kikwete alizishukuru
taasisi hizo kwa kufanya kazi Tanzania ili kusaidia taifa kufikia malengo
yaliyowekwa kwenye dira ya taifa kuhusu masuala ya afya. Alihimiza
ushirikiano na taasisi nyingine za Kitanzania hususan kwenye masuala ya
uhamashaji, utoaji wa elimu na kujenga uwezo kwa Watanzania kwenye masuala
ya lishe.
Akijibu swali la mtaalamu wa usalama wa chakula na lishe kutoka USAID Bi.
Laura Birx, Mama Salma Kikwete alisema msaada mkubwa unaohitajika kwa
Watanzania ni rasilimali fedha na elimu ili kuinua hali ya lishe kwa
watoto wa Tanzania.
“Kwenye maeneo mengi mijini, elimu kuhusu lishe ni muhimu zaidi kwani
baadhi ya familia wanauwezo wa kifedha na wanachohitaji sana ni elimu
kuhusu lishe” Alisema Mama Kikwete.
Hii inatokana na hali ya maisha ya mjini ambapo wazazi wengi wanajikita na
kazi na kuacha walezi wa nyumba kufuatilia lishe ya watoto. Alisema elimu
kwa walezi hao ni muhimu sana ili kuhakikisha kuwa watoto hao wanapewa
lishe bora.
Hivi karibuni USAID kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yasiyo ya
kiserikali imetoa fedha $ 30 milioni kutekeleza mpango wa lishe Tanzania.
Mpango huo ujulikanao kama Mwanzo Bora Nutrition Program unatekelezwa
kwenye mikoa mitatu ya Manyara, Morogoro na Dodoma kwa kipindi cha miaka
mitano. Mpango huo utakapokamilika utasaidia Serikali kujenga uwezo wa
kutoa elimu kuhusu lishe, kuinua hali ya lishe ya watoto wadogo, wakina
mama wajawazito na wanaonyonyesha.
Mkutano wa Mama Salma Kikwete na taasisi hizo ulioratibiwa na Africare kwa
kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Marekani, umefungua milango ya
ushirikiano baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na taasisi
hizo sita ili kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu umuhimu wa afya bora na
lishe kwa watoto.
Kwenye ziara hiyo, Mama Kikwete na ujumbe wake pia walitembelea Hospitali
Kuu ya Watoto Washington DC ya Children’s National Medical Center na
kutembelea wodi ya watoto wenye mahitaji maalum. Wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo kwenye masuala ya Uhusiano ya Kimataifa Dkt
Jerome Paulson alikubaliana na Dkt Hadija Hemedi Mwamtemi, Mkuu wa Idara
ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuanza mazungumzo ya
kushirikiana kwenye kuelimisha walimu (Training of trainers)
watakaofundishwa wengine kuhusu afya ya msingi kwa watoto ili kujikinga na
magonjwa yatokanayo na uharibifu wa mazingira.
Dkt. Paulson alisema mpango huo wa kutoa elimu kwa watoa huduma ya afya
kwa watoto hauna gharama kubwa lakini matunda yake yataonekana kwa kuwa na
watoto wenye afya bora baada ya kuwalinda na magonjwa kama vile pumu
yatokanayo na uchafuzi wa hewa.
Kwa upande wake Mama Salma Kikwete aliwasihi washirikiane na Chama cha
Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili
kwa pamoja kuanzisha mpango huo wa kubadilishana uzoefu na kupeana ujuzi
(TOT) ili kulinda afya ya watoto wa Tanzania.
Mama Salma Kikwete alifanya ziara hiyo wakati Rais Kikwete akihudhuria
Mkutano wa mwaka kuhusu Kilimo na Usalama wa Chakula Duniani Washington
DC, Marekani.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania, Washington DC
19.05.2012
No comments:
Post a Comment