Na Wilbert Molandi
LICHA ya kuchapwa kwa TKO, bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, amesema anataka kurudiana kwa mara nyingine na Francis Cheka.
Bondia huyo Jumamosi iliyopita alichapwa na kusalimu amri kwa kunyoosha mikono katika raundi ya saba kutokana na kushindwa kumudu kuendelea na pambano hilo lililopigwa kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatano, Maugo alisema kama promota wa kuandaa pambano lingine la marudiano dhidi ya Cheka atajitokeza, atapambana naye.
Maugo alisema alichapwa na mpinzani wake huyo kwa bahati mbaya lakini amepanga kufanya maandalizi ya nguvu kwa ajili ya kulipa kisasi ikiwezekana hata Julai, mwaka huu.
“Sioni sababu ya mimi kushindwa kurudiana na Cheka, ngumi ni mchezo wa makosa, ninaweza nikajirekebisha na kumpiga.
“Nipo tayari kurudiana naye ikiwezekana hata Julai, mwaka huu na alinipiga kwa bahati mbaya, sijakata tamaa,” alisema Maugo.

No comments:
Post a Comment