MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba ya urithi inayomilikiwa na Tatu Thadeo (37), mkazi wa Keko Machungwa pamoja na mali zote zilizokuwamo ndani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kuwa moto huo ulizuka juzi saa 2.00 usiku katika maeneo ya Keko Mwanga na kuteketeza chumba cha watoto pamoja na mali zote zilizokuwamo ndani.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa uliokuwa umewashwa na Abuu Ashiru ambao baadaye ulishika na kusambaa sehemu kubwa.
Misime alisema kuwa moto huo ulizimwa na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.
Alisema kuwa haukuwa na madhara zaidi kwa binadamu na upelelezi unaendelea ili kufahamu thamani halisi ya mali iliyoteketea.
Wakati huo huo watu 11 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kupatikana wakiwa na misokoto 16 ya bangi, puli tatu pamoja na lita 15 za pombe haramu ya gongo.
Watuhumiwa hao walikamatwa juzi kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Keko, Tandika na Kigamboni na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment