ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 5, 2012

Polisi yasomba wapigadebe Posta Mpya


Juu na chini ni WAPIGADEBE wanne wamekamatwa katika kituo cha mabasi cha Posta Mpya kwa tuhuma za kuwabughudhi abiria kituoni hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema wapiga debe hao walikamatwa juzi saa 10 jioni katika msako wa polisi uliofanywa katika maeneo mbalimbali ya Ilala.
Kamanda Shilogile aliwataja watuhumiwa hao ni Joseph James (22), Joseph Gidion (18) Magumu Kichumu (32) na Wilson Martine (25).
Katika tukio lingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke David Misime, wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na puli mbili za bangi .
Kamanda Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanywa na polisi, katika maeneo hayo.
Aliwataja watuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Hassan Abdallah (35) pamoja na Rajabu Adamu (31) wote wakazi wa mkoa huo.

 Habari Leo

No comments: