ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 8, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AMTEUA BI MWANAHAMISI OMARI KUWA MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII


Rais Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2012

No comments: