ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 4, 2012


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Mei 4, 2012, amemteua Bibi Saada Mkuya Salum kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi huo unaanza mara moja.
Rais amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Ibara ya 66 (i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa.
Chini ya Ibara hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapewa mamlaka ya kuteua wabunge 10 kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mpaka sasa, Rais Kikwete ameteua wabunge saba. Novemba mwaka 2010, aliteua wabunge watatu na jana, Alhamisi, Mei 3, 2012 ameteua wabunge wengine watatu ambao ni Professa Sospeter Muhongo, Bibi Janet Mbene na Bwana James Mbatia.

Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.Dar es Salaam.4 Mei, 2012

No comments: