ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 30, 2012

SHUKRANI TOKA TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC. USA

May 28, 2012


Tawi la CHADEMA Washington DC.
           
            Kwa niaba ya uongozi wa tawi la CHADEMA Washington DC. napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wote walio hudhuria ufunguzi wa tawi la CHADEMA uliofanyika Tarehe 27 May 2012 Washington DC nchini Marekani katika ukumbi wa Mirage Maryland.
            Aidha nawashukuru wageni waalikwa, Naibu katibu mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe, Mbunge wa Viti maalum kutokea Jimbo la Kwimba Mama Leticia Nyerere, Mbunge wa Iringa mjini Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nassari na Mbunge wa Viti maalum kutokea Zanzibar Mh. Mariam Msabaha kwa kutumia muda wao wa thamani kukaa na watanzania tuishio Marekani kubadirishana mawazo na kutuelezea mstakabari wa nchi yetu (Mama Tanzania) kijamii, kiuchumi na kisiasa.
            Mwisho napenda kuwashukuru watanzania wote walio hudhuria mkutano huu. Kwa kweli tumefarijika sana kuona utayari wa mioyo yenu kutaka mabadiliko (M4C) na uwazi wa kujielezea mawazo yenu bila kua na hofu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.

Asanteni sana kwa ushirikiano usio na mipaka


Katibu Mkuu-CHADEMA WASHINGTON DC

Liberatus Mwangombe

No comments: